Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, meneja wa Oxford hapa nchini Fatma Shangazi alisema uzinduzi huo ni miongoni mwa maazimisho ya miaka 50 ya kuwapo kwa chuo hicho hapa nchini.
Amesema vitabu hivyo vimefuata mukhtasari wa elimu wa mwaka 2016.
Amefafanua kuwa pia vimezingatia Sera ya elimu ya Taifa ambayo imeeleza wanafunzi wapimwe kwa weledi badala ya kukaririshwa.
"Kila inapoanza hatua nyingine ya somo, kuna maelekezo ya malengo ya somo na jinsi ya kumshirikisha mwanafunzi," amesema Shangazi.
Shangazi amefafanua vitabu hivyo ni vya somo la Kiingereza na Kiswahili kwa wanafunzi wa darasa la tatu na la nne, huku wa darasa la kwanza na la pili ni vya kusoma, kuandika na kuhesabu.
Kwa upande wa mwalimu Purity Mbiti ambaye ameshiriki katika uandishi wa vitabu hivyo amesema kuwa vinamvutia mwanafunzi kutokana na kutumia michoro ya kuvutia.
"Kwa kiasi kikubwa tulilenga kumshirikisha mtoto kwa kila hatua badala ya kumkaririsha," amesema Mwalimu Mbiti.
No comments:
Post a Comment