Wednesday, August 30

Mufti aagiza taasisi ya Twaiba kuwatendea haki mahujaji

Mwenyekiti wa taasisi ya Twaiba, Abubakar

Mwenyekiti wa taasisi ya Twaiba, Abubakar Mwinyi akizngumza na wanahabari. Amewaomba  radhi waumini wote waliopata usumbufu uliojitokeza akisema watasafiri kwenda Hijja mwakani. 
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ameitaka taasisi ya Twaiba kuhakikisha haki ya waumini iliowakwamisha kwenda hija Makka, Saudi Arabia inapatikana.
Pia, amewataka waumini hao wapatao 100 kuwa na subira.
Mjumbe  wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Sheikh Issa Othaman kwa niaba ya Mufti amesema kikao kinaendelea na atatoa tamko la mwisho kitakapomalizika.
"Mufti amenitumia nizungumze nanyi kwa kuwa mnataka taarifa, maongezi yamefikia pazuri, hivyo waumini wa Kiislamu na mahujaji kwa jumla wasiwe na shaka juu ya haki zao,” amesema Sheikh Othaman.
Amesema tangu jana Agosti 28, Mufti alichukua taarifa za pande zote na kuahidi haki zao zitapatikana.
"Hakuna haki ya mtu itakayopotea na pande zote wapo katika mazungumzo na bado yanaendelea, hivyo tusubiri kauli ya mwisho. Sababu za udanganyifu hazijawekwa bayana," amesema.
Mwenyekiti wa taasisi ya Twaiba, Abubakar Mwinyi amewaomba radhi waumini wote waliopata usumbufu uliojitokeza akisema watasafiri kwenda Hijja mwakani.
Alipoulizwa na waandishi wa habari sababu za kushindwa kuwasafirisha waumini hao, alikaa kimya.
Waumini hao walikwama kusafiri Agosti 23 baada ya taasisi ya Twaiba iliyoandaa na kuratibu safari yao kuelezwa kuwafanyia udanganyifu baada ya kuchukua fedha zao.
Kwa takriban siku tatu walikwama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment