Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea amevipongeza vikundi saba vilivyoiwezeshwa na Mfuko wa Mbunge kwa kuweza kujiendeleza na kuanza kufikia malengo waliyojiwekea.
Aliyasema hayo katika ziara ya vikundi saba katika kata nne za Wilaya ya Temeke akiwa ameongoza na wawakilishi kutoka Taasisi ya Global Patner ya nchini Uingereza.
Katika kata nne alizotembelea, Mtolea amewaonyesha wageni hao namna wananchi wanavyojikita katika kujiiunua kiuchumi kwa kuunda vikundi vyao binafsi na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ufugaji wa kuku wa mayai, kutotoa mayai, upandaji na uuzaji wa miti aina mbalimbali, na sanaa za mikono kama batiki, vikoba na masuala ya sanaa ya uigizaji.
Mtolea allitembelea kata ya Mtoni, Azimio, Vituka, Makangarawe na Kilakala
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Mtoni katika Kikundi cha Mfendengeni wanaojishughulisha na shughuli za upandaji wa vitalu vya miti ikiwa ni katika mradi unaosimamiwa na ofisi ya Mbunge.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Mtoni katika kikundi cha Naukalandima kinachojishughulisha na masuala ya utengenezaji samani za ndani (sofa) ikiwa ni katika mradi unaosimamiwa na ofisi ya Mbunge.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Azimio katika kikundi cha Saccos ya Vijana kinachojishughulisha na mradi wa utotoleshaji wa mayai ya kuku.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mtongani Unguja Kata ya Azimio akishuhudiwa na Mweyekiti wa Mtaa huo Zainab Liganja wakati wa ziara ya Mbunge huyo katika Miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata saba za Wilaya ya Temeke.
Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mtongani Unguja Kata ya Azimio akishuhudiwa na Mweyekiti wa Mtaa huo Zainab Liganj
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea.kata ya Azimio akimuonesha moja ya miradi ya kisima cha maji ambayo Ofisi yake inasimamia kikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Makangarawe katika kikundi cha Bongo Arts kinachojishughulisha na sanaa za Filamu na utengenezaji ikiwa ni katika moja ya miradi ya kuinua wakinamama na vijana katika ujasiriamali.
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akipokea risala kutoka kwa Katibu wa kikundi cha Tuna Utu Saleh Idrisa katika kata ya Kilakala kinachojishughulisha na ufugaji wa kuku na tayari wakiwa na kuku 1000 wa mayai ikiwa ni katika moja ya miradi ya kuinua wakinamama na vijana katika ujasiriamali.Chini ni mradi huo wa kuku.Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa pamoja na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kikundi cha Tekavi katika kata ya Vituka kinachojishugulisha na na sanaa za mikono ikiwa ni katika moja ya miradi ya kuinua wakinamama na vijana katika ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment