Polisi nchini Finland wanasema wanachunguza shambulio la visu lilofanywa jana, katika mji wa Turku kusini mashariki mwa nchi na wanachukulia tukio hilo kuwa la kigaidi.
Watu wawili waliuawa, na wanane wengine kujeruhiwa watatu wakiwa mahututi.
Polisi wamemtambua mshukiwa kuwa kijana wa miaka 18 kutoka Morocco.
Plisi wanasema, inaonyesha aliwalenga hasa wanawake, na wanaume aliowashambulia ni wale waliojaribu kumzuia.
Watu wengine wane wamekamatwa, kuhusu shambulio hilo, na amri imetolewa kimataifa, ya kumsaka mtu mwengine wa tano.
Wote wanasemekana kuwa na asili ya Morocco.
No comments:
Post a Comment