Mahakama kaskazini mwa India, imempa ruhusa mwanamke katika jimbo la Rajasthan ruhusa aachwe na mumewe, kwa sababu nyumba yao haina choo.
Wakili wa mke, alidai kuwa kwa vile mume hakumjengea choo ndani ya nyumba, katika miaka mitano ya ndoa, basi huo ni ukatili.
Jaji alisema kwenda kufanya haja nje ni kitu cha aibu, na ni kumuadhibu mwanamke, kukosa kumuweka mwanamke pahala salama anapokwenda haja.
Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa karibu nusu ya watu nchini India, karibu watu milioni 600 hawana choo.
Mwaka uliopita mwanamke alikataa kuolewa na mwanamume mmoja katika jimbo la Uttar Pradesh baada ya mwanamume kukataa kujenga choo.
No comments:
Post a Comment