Wednesday, August 9

MGOMBEA URAIS TFF, SHIJA RICHARD AANZA KAMPENI RASMI

Na Agness Francis, Globu ya Jamii
Mgombea wa Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Shija Richard ameanza rasmi harakati za kufungua kampeni yake ya kuwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo hapa nchini. 

Shija amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam nia na madhumuni ni kufungua rasmi zoezi la kampeni yake ambayo imejikita  kuzungumzia sera zaidi ya TFF  badala ya  maswala ya kiutendaji

Mgombea huyo amesema kuwa atahakikisha  kunakuwepo na sport Academi katika kanda sita hapa nchini, hii itaongeza vipaji vingi vya kabumbu na  kuwashawishi  wazazi wanapeleka watoto wao wenye vipaji katika  shule hizo za mafunzo ya mpira.

Hata hivyo Shija amesema kumekuwa na tatizo kubwa kwa klabu kukosa kuwa na uwanja, na hilo pia husababisha kutofanya vizuri kimataifa hivyo amesema atahakikisha anatafuta wadhamini kujikita katika swala zima la miundo mbinu ili kila klabu kujengewa kiwanja chake

Amesema ili kucheza mpira kwa amani na utulivu bila kupendelea upande mmoja wa timu  ataweka mkakati kwa kushirikiana na vyama vingine vya michezo duniani kote ili kuleta ufanisi kwenye mchezo huo hapa nchini.

Uchanguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti  mwaka huu mjini Dodoma ambapo wagombea hao wa  kiti cha urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) ni Shija Richard, Wallace Karia, Iman Madega, Ally Mayay,  na Emmanuel Kimbe.
Mgombea urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Shija Richard akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna atakavyofanya kampeni zake alizozizundua leo rasmi na akiahidi maendeleo ikiwemo na kujenga shule za akadeni ya kabumbu katika kanda sita 6 nchini.

No comments:

Post a Comment