Saturday, August 26

Mahakama yakataa kuondoa marufuku ya mifuko ya plastiki Kenya

Mifuko ya plastiki
Image captionMifuko ya plastiki
Mahakama kuu nchini Kenya imepinga jaribio la kusistisha marufuku ya mifuko ya plastiki inayotarajiwa kutekelezwa siku ya Jumamosi.
Watengenezaji wa mifuko hiyo wanasema kuwa hatua hiyo itasababisha watu 8000 kupoteza kazi zao iwapo marufuku hiyo itatekelezwa.
Akitoa uamuzi huo mahakamani, jaji alisema kuwa kuondoa marufuku hiyo kutaathiri kwa kiasi kikubwa sheria za usimamizi wa mazingira huku akisisitiza kuwa uhifadhi wa mazingira ni muhimu kuliko maslahi ya kibiashara.
Matatizo ya taka ya makaratasi ya plastiki nchini Kenya
Image captionMatatizo ya taka ya makaratasi ya plastiki nchini Kenya
Watengenezaji wa mifuko ya plastiki pamoja na wafanyibiashara wa mifuko hiyo walienda mahakamani wakipinga ilani iliotolewa na serikali inayopinga utengenezaji na uagizaji wa mifuko ya plastiki kutoka nje.
Walidai kwamba serikali itawaachishwa kazi maelfu wa raia mbali na kuathiri uchumi wa taifa hilo.
Hili ni jaribio la tatu katika kipindi cha miaka kumi kwamba Kenya imejaribu kupiga marufuku mifuko ya plastiki.
Jamaa na mzigo wa mifuko tele ya Plastiki Jijijini Nairobi
Image captionJamaa na mzigo wa mifuko tele ya Plastiki Jijijini Nairobi
Wizara ya mazingira inasema kuwa mtu yeyote atayepatikana akitengeza ama kufanya biashara ya mifuko ya plastiki atahudumia kifungo kisichopungua mwaka mmoja ama faini isiopungua dola 19, 000 za Marekani.
Kenya itajiunga na mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepiga marufuku mifuko ya plastiki ikiwemo Rwanda na Eritrea.

No comments:

Post a Comment