Ripoti ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ugonjwa wa Malaria hapa Nchini, inaonesha Kupungua kwa Maambukizi ya Maradhi Malaria Kwa Wastani wa asilimia 50 tangu Mwaka 2000.
Wakati Maambukizi yakionesha kupungua, inakadiriwa asilimia 90 ya Watanzania Wanaishi kwenye maeneo ambayo kuna maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria.
Kiongozi wa Uchunguzi na Matibabu kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Dkt Sixbert Mkude akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam amesema pamoja na ugonjwa wa Malaria umekuwa ni changamoto kwa sababu unazishambulia zaidi kaya masikini.
Dkt Sixbert Mkude amesema udhibiti wa Malaria na vifo vinavyosababishwa na Mbu waenezao vimelea vya Ugonjwa ni kuendelea na mikakati ya kutokomeza maradhi hayo.
Kwa upande wake Kiongozi Mdhibiti wa Mbu aneezae Malaria kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Charles Mwalimu amesema Sababu zinazokwamisha jitihada za kuukabili ugonjwa huo , Ikiwemo jamii kuwa na mwitikio hasi kwenye matumizi ya afua zinazotolewa na Serikali.
“Mpango wa Taifa wa Kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini, mwaka huu Serikali imepanga kuendelea na kampeni ya kupulizia viutalifu ukoko Kwenye Baadhi ya Wilaya zilizopo kanda ya ziwa” amesema Mwalimu
Kiongozi wa Uchunguzi na Matibabu kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Dkt Sixbert Mkude akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya Ugonjwa wa Malaria jinsi ulivyokuwa changamoto kwa sababu unazishambulia zaidi kaya masikini.
Kiongozi Mdhibiti wa Mbu aenezae Malaria kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria nchini, Charles Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuendelea kufuatilia tabia, wingi, Aina, Uwepo wa vimelea na usugu wa mbu ili kupanga mikakati ya kuutokomeza ugonjwa huo.
Wadau mbalimbali wa Afya wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
No comments:
Post a Comment