Handeni. Maagizo aliyoyatoa Rais John Pombe Magufuli alipokuwa kwenye ziara yake wilayani Handeni kwa mkandarasi aliyejenga mabwawa ya Maji ya Manga na Mkata kurudia ujenzi huo kutokana na kuyajenga chini ya kiwango yameanza kuchukuliwa hatua.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alisema wakandarasi ambao wametakiwa kufika eneo la ujenzi kwa siku 14 tayari ameshawaandikia barua kwa kutakiwa kufika eneo la kazi kwa siku tano kuanzia tarehe iliyopangwa.
Gondwe alisema agizo hilo linafanyiwa kazi kwa ushirikiano na viongozi wote na kuhakikisha kila agizo lililotolewa linafanyika kwa wakati uliopangwa na endapo itatokea kinyume na hapo kamanda wa polisi atafanya kama aliyoagizwa na Rais Magufuli.
“Wakandarasi hawa, wale ambao wanatakiwa kufika site (eneo la kazi) kwa siku 14 kamanda wa polisi wa mkoa analifahamu hilo na tayari nimeshamuelekeza mkurugenzi na amesha waandikia barua ya kufika kuja kufanyakazi kama mheshimiwa Rais alivyosema na fedha zao bado tumezishikilia hadi pale watakapokuja kufanya kazi na sisi turudishe taarifa kama tulivyoagizwa,”alisema Gondwe
Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Handeni, William Makufwe alisema tayari wameshawandikia barua wakandarasi hao na kuwataka kuwasilisha mpango kazi wao na gharama watakazotumia pia kwa kufuata ule wa awali wa mwezi wa tatu wa jinsi ya kurekebisha miradi hiyo.
No comments:
Post a Comment