Hivi karibuni Lissu amegoma kutoka ndani ya mahakama kwa madai kuwa polisi wanamvizia kumkamata mara baada ya kutoka mahakamani hapo mara baada ya kumalizika kwa kesi ya Chama cha Walimu Nchini (CWT) Manispaa ya Dodoma ambayo yeye ni wakili.
Tukio hilo lilitangazwa na vyombo vya habari TV, radio, magazeti na mitandao ya jamii ikimuonyesha Wakili huyo akizungumza ndani ya ukumbi wa mahakama, jambo ambalo inadaiwa liliwakera viongozi wa mhimili huo.
Hata hivyo, Lissu alitoka katika ukumbi huo mara baada ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Lazaro Mambosasa kumfuata na kumhakikishia hawana mpango wa kumkamata.
Ukaguzi wa watu wamebeba nini katika mabegi yao huanzia kwa walinzi getini ambao husimamia utaratibu wageni wanaoingia ndani ya uwanja wa mahakama hizo hasa baada ya kujua mgeni ni mwandishi wa habari.
“Kuna nini humu ndani ya begi ? Mmesoma yale mabango pale hairuhusiwi kupiga picha humu?,”alisikika mmoja wa walinzi wa mahakama hizo akimuuliza mwandishi wa habari aliyebeba begi lenye kamera.
Baada ya kujibiwa kuwa kuna kamera ndani ya begi na kumweleza kuwa anafahamu kuhusu katazo hilo na kwamba anaenda kwa uongozi wa mahakama kuomba kibali cha kupiga picha, alisindikizwa na mlinzi huyo hadi kwa naibu Msajili wa Mahakama.
Naibu Msajili Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Meseka John Chaba amemtaka mwandishi wa habari kuongozana na mlinzi huyo kila anapotaka kupiga picha katika eneo hilo mahakama.
“Ukitaka kupiga picha, umwite mlinzi na hakuna kufanya mahojiano ndani ya viwanja hivi. Huyu (anamuonyeshea mlinzi) hata akifanya kinyume na kukimbia najua tutamkamata tu,”amesema Chaba.
Hatua hiyo ambayo ni tofauti na utaratibu unaotumika katika mahakama nyingine nchini umekuja baada ya tukio la Lissu kugomea mahakamani na kujibu maswali ya waandishi ndani ya ukumbi wa Bunge.
Mmoja wa waandishi wa habari mkoani hapa, Danson Kaijage alisema kila mwandishi anayeandika habari za mahakamani amepata mafunzo juu ya kuandika habari za mahakamani ambazo zinakataza kurikodi ama kupiga kupiga picha wakati kikao cha mahakama kikiendelea.
“Sisi tumefundishwa hakuna kurikodi wala kupiga picha wakati mahakama ikiendelea jambo ambalo tunalizingatia sasa haya masharti mengine yanatupa usumbufu mkubwa katika kutekeleza majukumu yetu,”alisema.
Amesema nchi nyingine kama Kenya zinaruhusu kupiga picha wakati wote lakini waandishi wa habari wanatii hilo la kutopiga picha wakati kikao cha mahakama kinaendelea.

No comments:
Post a Comment