Saturday, August 5

Kagame aibuka kidedea


Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana Ijumaa nchini humo.
Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura ambazo tayari zimeshahesabiwa hadi hivi sasa.
Ushindi huo unamaanisha kuwa Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa ataendelea na awamu ya tatyu ya miaka saba.
Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuawa.
Wapinzani wa Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana.

No comments:

Post a Comment