Katika barua ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, Mrakibu mwandamizi wa polisi (SSP),E.Tille ambayo imethibitisha na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,(SACP) Charles Mkumbo imeeleza kuwa, Lema amezuiwa kufanya mkutano kuanzia kesho Agosti 27 hadi Septembaa mosi.
"Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yeye ratiba kuanzia Agosti27 hadi Septema mosi kwa ajili ya kupisha maandalizi ya kuhitimisha mtihani wa darasa la saba na mwenge wa uhuru" ilisomeka barua hiyo na kushauri Lema kupanga mikutano kuanzia Septemba 8 mwaka huu.
Kamanda Mkumbo amesema, sababu kubwa ya kuzuiwa mikutano hiyo ni kwa kuwa wanahitajika polisi wa ulinzi na hivyo haiwezekani kupata polisi wa kulinda mikutano na pia kushiriki katika masuala ya mitihani na mwenge.
"Haya ni mambo ya kitaifa hivyo ndio sababu OCD amesitisha mikutano ya mbunge na mambo haya yakimalizika ataendelea na mikutano yake"alisema.
Akizungumza na mwananchi jana, Lema alisema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwani ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.
Lema amesema sheria ya bunge kifungu cha nne fasihi ya kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.
Lema amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama baada ya kubainika katika mikutano zaidi ya 10 ambayo amefanya katika jimbo la Arusha imekuwa na mafanikio makubwa na wananchi wa Arusha wamepata fursa ya kujua ukweli wa mambo mbali mbali.
"Hizi ni njama najua walipanga kuvuruga mikutano na kuharibu vyombo vyangu wakashindwa, wakanitakama kwa kuzidisha dakika 7 kwenye mkutano wangu mmoja nikawashinda kwa hoja sasa wameona wazuie kabisa na ikiwezekana watumie nguvu"alisema
Amesema sasa anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi ama aendelee na mikutano kwani kimsingi, maeneo ambayo mikutano imepangwa kufanyika sio ya shule .
"Sasa kesho Jumapili nipo nje ya mji eneo la Olmoti kuna maandalizi yapi ya mwenge na darasa la saba , ntakuwa na mkutano eneo la soko la Shuma kuna mkusanyiko kila siku wa watu, nitaathiri nini huo mwenge ambao utafika kuanzia Septemba 6"amesema
Hata hivyo amesema, baada ya barua hiyo na kushauriana na mawaziri kadhaa na viongozi wa serikali, atalifikisha pia bungeni, kwani ni jambo la ajabu mbunge kuzuiwa kufanya mikutano kwasababu za mwenge na mitihani ya darasa la saba.
Amesema muda ambao umetakiwa na polisi afanye mikutano, anapaswa kuwa katika shughuli za kibunge jambo ambalo anaamini litaathiri ratiba za utendaji wa kazi zake.
No comments:
Post a Comment