Wednesday, August 30

Je wajua ndege hutumia harufu kusafiri maeneo ya mbali?

Ndege kwa jina Arctic turn uhamia maeneo yalio umbali wa maelfu ya kilomita bila kupotea.Haki miliki ya pichaB. G. THOMSON/SCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionNdege kwa jina Arctic turn uhamia maeneo yalio umbali wa maelfu ya kilomita bila kupotea.
Ndege uhamia maeneo yalio umbali wa maelfu ya kilomita bila kupotea.
Kwa mfano ndege kwa jina Arctic yeye huwa Uingereza majira ya joto na baadaye kusafiri hadi eneo la Atarctic wakati wa majira ya baridi.
Licha ya hayo yote kufanyika , wanasayansi bado hawajui ni vipi ndege husafiri kwa umbali huo wote na kuwasili katika maeneo wanayoelekea kila mwaka bila kupotea.
Kulingana na utafiti mpya, harufu hutumika kama kiungo muhimu wakati ndege hao wanapohamia maeneo mengine yalio mbali wakiwa juu ya bahari.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford, Barcelona na Pisa kwa makusudi waliwatoa viungo vya mwili vinavyobaini harufu ndege hao kabla ya kufuatilia wanakoelekea.
Walibaini kwamba wanaweza kusafiri juu ya ardhi lakini wanaonekana kupotea wanapopaa juu ya bahari.
Hatua hiyo ilibaini kwamba hulazimika kutumia ramani ya harufu kutafuta njia ya wanakoelekea wakati ambapo hawaoni cha kutegemea.
Vipimo vya awali vilionyesha kuwa unapowatoa ndege hao viungo wanavyotumia kutambua harufu unawazuia kuweza kurudi walikotoka.
Hatahivyo wengine walikuwa na maswali ya iwapo unapowatoa viungo hivyo unaweza kulemaza uwezo wao wa kutafuta chakula.
Utafiti mpya unaondosha pingamizi hizo, na kuonyesha kuwa itakuwa vigumu katika siku za usoni kuhoji kwamba hatua ya kutambua harufu haitumiki wakati ndege hao wanaposafiri maeneo ya mbali ,alisema mtafiti Oliver Padget wa idara ya elimu ya wanyama katika chuo kikuu cha Oxford.

No comments:

Post a Comment