Wazazi na ndugu waliruhusiwa kuingia ndani ya ndege hiyo kuwapokea watoto wao ambao wamepata nafuu kwa kiasi kikubwa.
Wilson Tarimo alikuwa wa kwanza kushuka katika ndege akiambatana na mdogo wake aliyeingia katika ndege kwa ajili ya kumpokea.
Baada ya hapo aliyefuatia ni Saidia Awadhi pili akifuatana na Doreen Mshana kushuka katika ndege hiyo iliyokuwa na wajumbe 16 ambao waliambatana na watoto hao.
Baada ya kushuka walipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliyeambata na viongozi wengine kutoka Mkoa wa Arusha.
Watoto hao wote wakati wanashuka walionekana wenye nyuso za furaha baada ya kukaa Marekani kwa miezi mitatu wakipata matibabu.
No comments:
Post a Comment