Faru kutoka familia ya wale walio kwenye hatari ya kuangamia ambaye alisombwa na mafuriko kutoka nchini Nepal hadi India ameokolewa na kurudishwa nyumbani.
Faru huyo wa kike alipatikana umbali wa kilomita 42 kutoka mbuga ya Chitwan iliyo kijiji cha Bagah.
Faru wengine wanne kutoka mbuga hiyo wanahitaji kuokolewa na mmoja tayari amepatikana akiwa amekufa.
Bonde la Chitwan nchini Nepal, iliyo mbuga ya wanyamapori ambayo ni makao kwa faru 600, imeathirika vibaya na mafuriko.
Wiki iliyopita ndovu kadha na mashua vilitumiwa kuwaokoa karibu watu 500 waliokuwa wamekwama eneo hilo.
Kundi la maafisa 40 wa Nepal walitumwa kumridisha nyumbani faru huyo wa umri wa miaka miwili unusu.
Mamia ya watu raia wa India walifika kutazama shughuli hiyo ya uokoaji.
Msimu wa mvua unaonza mwezi Juni hadi Septemba husababisha mafuriko kote eneo hilo kila mwaka.
Katika jimbo la Assam nchini India, faru sita wameripotiwa kufa maji kufuatia mafuriko katika mbuga ya Kaziranga.
No comments:
Post a Comment