Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (wa pili kulia) akizungumza na mmoja wa mafundi wanaojenga Jengo Jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Wa kwanza kushoto ni Mhandisi John Ainainyi Njau kutoka Benki ya Dunia - Tanzania.
Muonekano wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
Baadhi ya mafundi wakiwa wanaendelea na kazi ya ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) linalojengwa mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa waandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya ofisi hiyo mkoani Dodoma. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
No comments:
Post a Comment