Pichani ni dereva wa gari la mwendokasi la DARTS namba za usajili T.124 DGW akihojiwa baada ya kufanya kosa la kupita taa nyekundu eneo la Kibo barabara ya Morogoro jijini Dar es salaam leo asubuhi wakati akitokea Kimara kuelekea Kivukoni. Baada ya kukamatwa hatua za kufikishwa mahakamani zinaendelea.
salaam ACP Awadhi Haji amesema baada ya kumkamata dereva huyo kwamba baadhi ya madereva wa magari hayo wamekuwa wakifanya makosa ya usalama barabarani mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupita taa nyekundu, kutosimama kwenye vivuko vya waenda kwa miguu na kadhalika wakidhani kuwa wao hawawezi kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Hivyo naelekeza kuwa madereva hao wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali kama madereva wengine pindi wanapobainika kuvunja sheria za barabani" ameamuru ACP Awadhi Haji ambaye huwa hana masikhara awapo kazini.
No comments:
Post a Comment