Friday, August 11

CHANGAMOTO ZA WASANII WA NYIMBO ZA INJILI ZAWEKEWA MIKAKATI YA KUTATULIWA



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii wa Nyimbo za Injili (hawapo pichani) wakati wa mkutano na wasanii hao kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare akifafanua jambo wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba akiwasilisha changamoto zinazokabili muziki wa injili hapa nchini wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. 
Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bi. Christina Shusho akichangia hoja wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. 
Waimbaji wa nyimbo za Injili wakitumbuiza wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na viongozi kutoka serikalini pamoja na viongozi wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania baada ya mkutano na wasanii hao kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

…………………………….

CHANGAMOTO ZA WASANII WA NYIMBO ZA INJILI ZAWEKEWA MIKAKATI YA KUTATULIWA

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Tarehe: 10/08/2017

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe amekutana na wasanii wa nyimbo za Injili leo Jijini Dar es Salaam kusikiliza changamoto zinazoikabili tasnia ya muziki wa nyimbo za injili na kuweka mikakati ya kuzitatua changamoto hizo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mkutano na wanamuziki wa nyimbo za Injili Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali ina wajibu wa kufuatilia changamoto za tasnia ya muziki ukiwemo muziki wa injili na kuzitatua ili kuweza kukuza kazi za wasanii kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na taifa.

“Muziki ni tasnia ambayo imewabeba vijana wengi hapa nchini, serikali ina wajibu wa kutetea, kulinda na kuhakikisha maslahi ya kazi za sanaa ikiwemo muziki wa injili inaheshimiwa na kulindwa” Amesema Mhe. Mwakyembe

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare amewataka Wasanii wa Muziki wa Injili kutoshawishiwa kutoa malipo yoyote katika vyombo vya habari ili nyimbo zao ziweze kuchezwa kwenye vyombo hivyo bali vyombo vya habari ndio vinapaswa viwalipa wasanii wakati wanapotumia nyimbo zoa.

Aidha Bibi. Doreen amewaomba waimbaji hao wa nyimbo za injili kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu, Cosota na Basata ili waweze kupata ushauri wa namna ya kuandika mikataba bora na inayofaa wakati wa kutengeneza na kuandaa albamu za nyimbo za injili.

Naye Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba amewataka Viongozi wa nyimbo za Injili Tanzania kuhakikisha kuwa wanafanya kazi bega kwa bega na serikali na kwa bidii katika kukuza, kuendeleza, na kulinda maslahi ya wanamuziki wa Injili.

Aidha Bw. Novemba ameiomba serikali kuhusisha wanamuziki wa nyimbo za injili katika matukio mbalimbali ya serikali na ya nchi kwani wasanii wa nyimbo za injili wamekua wakiimba nyimbo zinazojenga taifa na kuendeleza amani, upendo na ushirikiano wa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment