Kwa nyakati tofauti, walisema hayo jana wakati wakitoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha kulelea watoto cha Yatima Group Trust Fund (YGTF).
Msaada huo wa mifuko ya saruji 35, sukari kilo 25, unga kilo 50, sabuni, vifaa vya watoto shuleni, nguo pamoja na mahitaji mengine yenye thamani ya Sh2 milioni, ni sehemu ya kuazimisha miaka 25 ya Chadema tangu kuanzishwa kwake.
Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Dar es Salaam, Magreth Mugyabuso alisema wanathamini hali ya watu wa chini hasa wenye uhitaji, ndiyo maana imewasukuma kuwapatia msaada ikiwamo vifaa vya shule ili kupata elimu bora.
“Watoto hawa wanahaki kama wengine ambao wanasoma, imetugusa kufanya haya Mkoa wa Dar es Salaam... suala la elimu lipewe kipaumbele hasa kwa watoto wa kike tukiamini ukimwelimisha msichana umeelimisha jamii,” alisema Mugyabuso.
Mbunge wa Viti Maalumu Ilala, Anatropia Theonest alisema hawawezi kwenda tofauti na kauli ya Mdee.
Aliitaka jamii iunge mkono suala la mtoto wa kike kurudi shuleni akipata ujauzito na kujifungua.
“Wasichana hawapati mimba kwa kujitakia, wengi wanapitia magumu, mfano katika halmashauri ya Ilala, miezi mitatu iliyopita watoto 156 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na watu wanaowazunguka. Jamii inapaswa kulikemea hili kwa kuwa matatizo humkuta kila mtu,” alisema Theonest.
Alisema kumnyima mtoto elimu ni kukiuka haki yake na misingi ya katiba ya nchi inayomtaka kila mtu apate elimu.
“Serikali inapaswa kuliangalia hili kwa makini, wengi wananyanyaswa wakiwa wadogo, hivyo bila kukemea baadhi ya kauli ni miongoni mwa ishara ya kuwakandamiza,” alisema.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Catherene Vallence alisema wanawapa kipaumbele wasichana na watoto wenye uhitaji katika kuhakikisha wanapata elimu bora huku wakiendelea kumuunga mkono Mwenyekiti wa Bawacha Taifa.
“Mwenyekiti Mdee, amepambana katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake na sisi hatuko nyuma, ndiyo maana tunatekeleza haya kwa kuwafikia wananchi wa hali ya chini,” alisema Vallence. Aliaema hata idadi ya wapigakura wengi ni wanawake na ndilo kundi kubwa linalotaka maendeleo, hivyo kwa kumnyima elimu ni njia ya kumkwamisha kufikia ndoto zake.
Mkurungenzi wa YGTF, Winfrida Lubanza alisema kituo hicho kina watoto 151.
Pia, alisema wengine 300 waliokuwapo kituoni hapo wameondoka baada ya kumaliza shule na kuajiriwa.
No comments:
Post a Comment