Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aamuru ofisi za kituo cha habari cha al Jazeera kufungwa mjini Jerusalemu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa amri ya kufungwa kwa ofisi za kituo cha habari cha kimataifa cha al Jazeera mjini Jerusalem.
Ukandamizwaji wa waandishi wa habari na vyombo vya habari na jeshi la Israel mjini Jerusalem umeathiri kituo cha habari la al Jazeera.
Waziri mkuu wa Israel katika kurasa zake katika mitandao ya kijamii amesema kuwa ameamuru kufungwa kwa ofisi za kituo cha al Jazeera kwa kuwa kinashawishi ghasia katika mskiti wa al Aqsa.
Wanahabari wanoajaribu kunasa picha za matukio ya ghasia al Aqsa hushambuliwa na kubugudhwa na jeshi la Israel.
No comments:
Post a Comment