Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma ameviasa vyuo vikuu nchini vizalishe wataalam ambao watakuwa msaada kwa taifa.
Waziri huyo ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya vyuo vikuu nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inasisitiza viwanda hivyo lazima vyuo vijenge dhana hiyo kwa kuzalisha wataalam wataofanya viwanda hivyo viwepo kutokana na ujuzi walionao.
Waziri Riziki ametaka vyuo vikuu kutokana na maonesho kuwa na mitazamo mipya ya kuwa na mitaala ambayo itazalisha wataalam wenye uwezo katika soko la ajira na hata kujiajiri.
Amesema kuwa serikali inaangalia vyuo vikuu vinavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na kuangalia utafiti kwa ajili ya maendeleo ya taifa pamoja na watu wote.
Nae Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Eleuther Mwageni amesema kuwa maonesho yajayo wataboresha na kuangalia uwezekano wa kuongeza siku kutokana na maoni ya wadau wa vyuo vikuu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya vyuo vikuu nchini katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Eleuther Mwageni akizungumza wakati maonesho ya vyuo vikuu nchini katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment