Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam Ijumaa amefanya Dua maalum kwa wakaazi wa Temeke na maeneo ya jirani katika uwanja wa Mwembe Yanga.
Dua hiyo ambayo imefunguliwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Musa itakuwa kwa siku tatu kuanzia Ijumaa tarehe 28-07-2017 mpaka Jumapili tarehe 30-07-2017 ambapo itafungwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda.
Dua ya Sheikh Shariff pamoja na kuliombea Taifa letu pamoja viongozi wake makini lakini pia ni maalum kwa wakazi wa Temeke ambao mara nyingi wamekuwa wakimpigia simu Sheikh mara kwa mara ili aende kufanya mkutano wa Dua kwa ajili ya utatuzi wa matatizo yao mbalimbali yakiwemo Majini na wachawi mbalimbali wanaowasumbua.
Dua za Sheikh huwa zinaanza mchana saa nane na kumalizika saa kumi na mbili jioni.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa akizungumza kwenye Dua hiyo iliyoendeshwa na Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam
Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam akiongea
Sheikh Shariff Majini kutoka kituo cha Dua na Maombi Mabibo Jijini Dar es salaam akimshukuru Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa
Sehemu ya umati wa kinamama wa Temeke na maeneo ya jirani waliohudhuria dua hiyo
No comments:
Post a Comment