Ni siku moja baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kumuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendelea na hatua zinazostahili kujaza nafasi za Wabunge waliofutwa uanachama na CUF kwa mujibu wa Sheria.
Leo July 27, 2017 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ‘NEC’ imefanya uteuzi wa Wabunge 8 wa Viti Maalum ambao wataziba nafasi za Wabunge ambao wamevuliwa uanachama na Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha July 27, 2017 imewateua wafuatao kuwa Wabunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi CUF.
No comments:
Post a Comment