Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa njia aliyoitumia aliyekuwa mgombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu uliopita kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ilikuwa ni aina fulani ya ufisadi wa kisiasa.
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifanya mahojiano na Gazeti la Mwananchi ambapo amesema kuwa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chadema njia aliyoitumia ilikuwa ni aina mojawapo ya ufisadi kwakuwa hakupitishwa na chombo chochote ndani ya chama chake.
Amesema kuwa hata katika Kampeni za uchaguzi mkuu, Ukawa haikuzungumzia suala la ufisadi kwakuwa kiongozi huyo teyari alikuwa ameshajiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
“Kwenye Kampeni za mwaka 2015 chama kikuu cha upinzani (Chadema) hakikuwa tena kinazungumzia suala la ufisadi, labda kwa hofu kuwa mshtumiwa wa ufisadi alikuwa mgombea wao, kwa bahati mbaya wao ndio waliibua tuhuma za ufisadi, lakini kuondoka kwa Dkt. Slaa nako kulikuwa ni tatizo, ingawa watu hawakutaka kulifuatilia,” amesema Mghwira.
No comments:
Post a Comment