MASHUJAA WA RIADHA WENYE HISTORIA NZITO ZA MICHEZO KULIKO ZOTE TANZANIA
Pichani ni Jenerali Mirisho Hagai Sarakikya (kati) akiwa na wanariadha mabingwa wa dunia wa zamani, Filbert Bayi (kushoto) na Juma Ikangaa. Hawa ni watu watatu ambao mjina yao yanastahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu katika vitabu vya kumbukumbu ya historia ya riadha na michezo nchini Tanzania. Hilo halina ubishi...
Tukianza na Jenerali Sarakikya, yeye ndiye alikuwa Mkuu wa Majeshi wa kwanza mara tu bada ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1964 na akatumikia wadhifa huo kwa miaka kumi yaani toka hiyo 1964 hadi alipostaafu mwaka 1974. Wakati anapata cheo kuwa CDF Jenerali Sarakiya pia alikuwa ndiye mwenyekiti wa chama cha riadha cha Tanzania (TAA) kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1972.
Ikiwa hiyo haitoshi mara baada ya kustaafu jeshini mwaka huo huo wa 1974, Mwalimu Nyerere alimteua Jenerali Sarakikya kuwa Waziri wa Michezo, Vijana na Utamaduni.
Ukiangalia katikati ya mistari utamaizi kwamba historia ya mafanikio ya riadha na michezo kwa ujumla nchini Tanzania yalikuwa katika miaka hiyo ambayo Jenerali Sarakikya alikuwa mwenyekiti wa TAA, Mkuu wa Majeshi na baadaye Waziri wa michezo, vijana na utamaduni.
Huo ndio wakati wanariadha Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Suleiman Nyambui, Gidamis Shaganga, Mwinga Mwanjala, Nzaeli Kyomo na wengi wengine walikuwa wanang’ara kwenye medani za kimataifa.
Kwa hiyo picha hii ni kubwa na yenye historia nzito kwa kadri mafanikio katika michezo kwa nchi hii yanahusika.
Wote watatu ni wanajeshi wastaafu, kwani Filbert Bayi baada ya ushindi wake alipandishwa cheo hadi kuwa Luteni, na baada ya kuhudhuria mafunzo ya afisa kadet huko Monduli mwaka 1977 alipanda kuwa Kepteni. Hadi anastaafu mwaka 2001 alikuwa na cheo cha Meja kitengo cha ufundi wa ndege jeshini.
Kwa upande wa Ikangaa, yeye alikuwa Mkurugenzi wa michezo makao makuu ya jeshi hadi alipostaafu kwa mujibu wa sheria akiwa na cheo cha Kanali.
Filbert Bayi Sanka ni mwanariadha aliyeiandikia Tanzania historia isiyoweza kusahaulika. Filbert Bayi ndie mwanariadha wa Pili ambae anakamilisha medali ya pili ya Tanzania kwenye Mashindano ya Olympic.
Tanzania Imewahi kupata Medali mbili tu katika Mashindano ya Olympic mpaka sasa. Filbert Bayi alipata Medali ya Silver katika mbio za mita 3000 katika mashindano ya Olympic yaliyofanyika mwaka 1980 MOSCOW Mwaka 1978(mita 1500) na Mwaka 1973 (mita 1500) katika mashindano ya All African Games Fibert Bayi alishinda Medali za Dhahabu kwa kuibuka namba moja katika mashindano yote 2.
Ushindi huu ulitengeneza historia kubwa Tanzania. Mwaka 1974 katika mashindano ya Commonwealth Games yaliyofanyika Christchurch “New Zealand” Filbert Bayi aliweka rekodi ya kukimbia mita 1500 kwa dakika 3 na sekunde 32.2 mbele ya mwanariadha kutoka New Zealand John Walker na Mkenya Ben Jipcho, hivyo kuiwezesha Tanzania kupata medali ya Dhahabu katika mashindano hayo. Video ya chini inakupa maajabu aliyofanya Juma Ikangaa.
No comments:
Post a Comment