Monday, July 17

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA (TCAA) YAWEKA WAZI SABABU YA KUZUIWA URUSHAJI WA DRONES


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Morogoro
  NDEGE zinazorushwa bila rubani kwa ajili ya kupiga picha (Drone) ni marufuku kutokana na msuala ya anga, Mwanasheria wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Bi. Maria Makalla amesema, wakati wa semina ya waandishi ya wahabari iliyofanyika mjini Morogoro mwisho mwa juma.
Semina hiyo ilihusu kuwaelimisha wanahabari hao juu ya majukumu ya TCAA pamoja na matokeo ya ukaguzi wa kimataifa baada ya Mamlaka hiyo kukaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO).
 Bi Makalla amesema ndege zisizo rubani hazitakiwi zirushwe kiholela kwani kama ilivyo sehemu zote duniani zinatakiwa kuwekewa kanuni kutokana na usalama wa anga.
"Wanaomiliki drones kwa sasa wasizitumie mpaka utaratibu mahususi wa namna ya kuzitumia utakapotoka, ikiwa  ni pamoja na mamlaka kujua wamiliki wote wa ndege hizo na jinsi ya kuzitumia.
"Drones ni ndege ndogo na zina athari kubwa endapo huko angani zitakutana na ndege nyingine na kusababisha ajali," amesema mwanasheria huyo wa TCAA.
Ameweka bayana kwamba utaratibu unaandaliwa  na kwamba wadau wote wanaomiliki drones itabidi kwanza  kuelimishwa masuala ya usalama wa anga na kujua kanuni zake zitazotungwana kutolewa  kwa mujibu wa sheria.
"Masuala ya anga ni mapana na kila siku teknolojia zinabadilika katika matumizi ya anga hivyo inatupasa sote kwenda kwa mujibu wa  kanuni za teknolojia hizo", alisema.
 Mwanasheria Mwandamizi waMamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Maria Makalla akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari juu ya majukumu ya  Mamlaka hiyo pamoja na matokeo ya ukaguzi wa kimataifa Mamlaka ilivyokaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wa semina iliyofayika mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina  hiyo iliyofayika mjini Morogoro mwishoni mwa juma.


 Meneja  Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), BestinaMagutu  (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya majukumu ya Mamlaka hiyo

Mwanasheria Mwandamizi waMamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Maria Makalla akiwa na 
 
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria semina ya majukumu ya  TCAA pamoja na matokeo ya ukaguzi wa kimataifa Mamlaka ilivyokaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wa semina iliyofayika mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina  hiyo iliyofanyika mjini Morogoro mwishoni mwa juma.

No comments:

Post a Comment