Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, kama ishara ya kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi. Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimshuhudia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, wakati wa kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi, Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo, (katikati) ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
No comments:
Post a Comment