Wednesday, July 19

KIMENUKA..Mchungaji Mwingira Ashtakiwa Kwa Kudaiwa Kuzini na Kuzaa na Mke wa Raia wa Marekani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeombwa kumwamuru Mchungaji Josephat Mwingira akapime kipimo cha kubaini vinasaba (DNA) ili kujua baba halali wa mtoto anayedaiwa kuzaa na Dk. Phillis Nyimbi ambaye ni mke wa Dk. William Morris.

Maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo, Dar es salaam jana na Dk. Morris kupitia wakili wake, Respicius Ishengoma.

Dk. Morris ambaye ni raia wa Marekani, alifungua kesi katika mahakama hiyo akimtuhumu Mchungaji Mwingira kuzini na kuzaa na mke wake Dk. Nyimbi.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakili Ishengoma aliwasilisha maombi hayo akitaka mteja wake, Dk. Morris na mkewe Dk. Nyimbi, Mchungaji Mwingira na mtoto aliyezaliwa, wakapime kipimo hicho ili kujua baba halali wa mtoto huyo mwenye umri miaka tisa sasa.

Katika maombi hayo namba 113/2017, Dk. Morris anaomba mahakama itoe amri wahusika wote wakapime DNA.

Baada ya kuwasilisha maombi hayo, mahakama imeyapokea na kutoa siku 14 kwa Mwingira kuyajibu kisha usikilizwaji uanze na kutolewa uamuzi. Mwingira atajibu Agosti 2,mwaka huu.

Katika kesi ya msingi namba 306/2013, Dk. Morris amewashtaki Mwingira na Dk. Nyimbi, na anadai alipwe fidia ya Sh bilioni 7.5 kwa mchungaji huyo kuzini na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mkewe.

No comments:

Post a Comment