Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo, Sanaa na Burudani, Dkt. Harrison Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan ya Jijini Dar es salaam.
Dkt. Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.
Dkt. Mwakyembe ametoa shukrani hizo Julai 26 wakati akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Kunduchi wilayani Kinondoni.
"Wanafamilia tutakumbuka moyo adhimu na upendo na ushirikiano tulioupata kutoka Katibu Mkuu wa wizara hii Profesa Elisante Ole Gabriel na viongozi wengine waandamizi wa Serikali. Mwisho kabisa Wanakyela kwa uvumilivu wao katika kipindi hiki kigumu," amesema Dkt. Mwakyembe.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki katika kumfariji kipindi cha msiba wa mke wake mpendwa Bi. Linah George Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment