Sunday, June 18


Southmpton. Je ni fedha kiasi gani zinaweza kukushawishi kukubali kuambukizwa kikohozi ili kusaidia uvumbuzi wa kisayansi?
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Southampton wamesema watampa pauni 3,526 (sawa na Sh10.3 milioni)  mtu yeyote atakayejitokeza ili kukubali changamoto hiyo.
Lengo lao kubwa ni ili kutengeza chanjo bora ili kuwalinda watoto na watu wazima ambao wapo hatarini kuambukizwa ugonjwa huo.
Ili kusaidia ni sharti mtu awe na umri wa kati ya miaka 18-45, awe na afya bora, awe tayari kutengwa kwa siku 17 na kuimba.
Kikohozi ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa haraka na huenezwa kupitia hewa ya kikohozi kutoka kwa mtu ambaye ameambukizwa.
Kundi hilo la watafiti wa Chuo Kikuu cha Southampton linataka kuwaambukiza watu walio na afya nzuri kwa kuwawekea puani viini vinavyosababisha maambukizi hayo na kuwachunguza.
 Baadhi ya watu waliojitolea watakuwa wagonjwa, lakini wanasayansi wanawataka wale ambao hawatakuwa na dalili zozote licha ya kuwekewa viini hivyo katika pua zao.
Hatu hii inalenga kujua wale wenye kinga ya asili ya ugonjwa huo.
 Vilevile, wapo wanaobeba ugonjwa huo kwa siri na huwaambukiza watu wengine, lakini huwa hawaambukizwi.

No comments:

Post a Comment