Chama hicho kimefikia hatua hiyo kwa kuzingatia ibara ya 17 ya katiba yake ambayo inatamka kuwa kiongozi wa chama atakoma kuendelea na madaraka yake iwapo atashindwa kutekeleza majukumu yake.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Kaimu Kiongozi wa ACT, Samson Mwingamba alisema kamati ya uongozi wa ACT ulikutana leo lengo kuu ni kutafakari lililotokea kuona namna gani Mgwhira anaweza kutimiza majukumu yake kama Mwenyekiti na Mkuu wa Mkoa.
“Kama chama baada ya kutafakari kwa kina na baada ya mashauriano baina yake na viongozi kutumia katiba ya chama anakoma kuwa kiongozi kwa kuwa kutakuwa na mgongano wa majukumu, maslahi hivyo anakoma kuwa mwenyekiti,” alisema Mwigamba.
Mwigamba alisema kamati ya chama imemchagua Yeremia Maganja kuwa Kaimu Mwenyekiti na kamati ilimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua Mgwhira.
Hata hivyo, Mwigamba alisema Mghwira bado ataendelea kuwa mwanachama halali wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment