Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amekutana na Masheikh na Viongozi wa Misikitini zaidi ya Mia sita (600) ya Mkoa wa Dar es salaam.
Hatua hii ni muendelezo wa Mikutano yake na Makundi ya watu mbalimbali, ambapo katika kuenzi mwezi wa Mfungo wa Ramadhani.
Mhe Makonda ametoa vitu mbalimbali kama SADAKA KWA KILA KIONGOZI vifuatavyo kwa kila Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam :-
1. Mchele Kg 25
2. Ngano Kg 25
3. Sukari Kg 25
4. Mafuta ya kupikia Lita 20
Akizungumza na Masheikh na Viongozi wa Dini ya KIISLAMU, Mhe Makonda kwanza amewapongeza kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali pamoja na kumuunga mkono Mhe, Rais, Dot. John Pombe Magufuli kwa jinsi ambavyo anatekeleza utendaji wake wa kazi kwa kuhakikisha anaipeleka Tanzania kwenye nchi ya Uchumi na kipato cha kati kupitia mapinduzi ya VIWANDA.
Mhe Makonda pia, amewaomba viongozi wa Dini kuutumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kuhubiri AMANI, UTULIVU NA KUVUMILIANA katika kila mambo wanayofanya waumini wao.
Katika hatua nyingi, Mhe Makonda amefanikiwa KUWASHAWISHI wafanyabiashara haswa wa SUPERMARKET Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi mpaka saa sita za usiku, ili kutoa fursa kwa wananchi kujipatia mahitaji yao muhimu kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
16/06/2017

No comments:
Post a Comment