Monday, April 13

HABARI KUBWA-ZITTO KABWE AENEZA UWONGO WAKE TENA,ATUMIA ZIARA YAKE KUUCHAFUA UKAWA MIKOANI,SOMA HAPA KUJUA



KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameendelea kuwadanganya wananchi kuwa kufukuzwa kwake katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kumetokana na umakini wake wa kufuatilia “mambo yanayowakandamiza wanyonge.” Anaandika Ditha Nyoni, Songea … (endelea).

Akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Ruvuma, Zitto amewadanganya wananchi kuwa kufukuzwa kwake Chadema, kumetokana na msimamo wake wa kutetea maslahi ya wananchi. Amesema baada ya kutambua baadhi ya viongozi wa Chadema hawataki kuwatumia wanyonge kwa kuwapigia kura na kujipatia ruzuku, yeye wenzake wengine wameamua kuanzisha chama kitakacho watetea wanyonge wakiwemo wakulima ambao nguvu zao zikiisha wanakufa maskini.

Amedai kuwa yeye ndiye aliyeibua hoja ya mkataba wa madini wa Buzwagi ambako waziri wa nishati na madini, alifutwa kazi; hoja ya kumng’oa aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa, Operesheni Tokomeza, wanaoficha fedha nje ya nchi na sakata la Escrow.
Amewataka wananchi madai kuwa yeye ni msaliti na kwamba wawapime wabunge wao kwa kazi walizozifanya. Hata hivyo, katika yote aliyoeleza Zitto hakuna hata moja ambalo ni kweli.

Mathalani, hoja ya mkataba wa Buzwagwi, iliibuliwa na gazeti la kila wiki la MwanaHALISI; katkka sakata la Buzwagwi, kinyume na madai yake, hakuna waziri hata mmoja aliyefutwa kazi. Aliyekuwa waziri wa nishati na madini, Nazir Karamagi ambaye alisaini mkataba huo nchini Uingereza, alifutwa kazi 18 Februari 2008, kutokana na kashifa ya maarufu ya Richmond. Sakata la Richmond liliibuliwa bungeni na Kamati ya Nishati na Madini iliyokuwa chini ya aliyekuwa mbunge wa Bumbului (CCM), William Shelukindo. Vilevile, kinachoitwa “Operesheni Tokomeza,” kiliibuliwa bungeni na Christopher ole Sendeka, mbunge wa Simanjiro (CCM).

Kamati Kuu (CC) ya Chadema, ilimfukuza uanachama Zitto na wenzake watatu – Prof. Kitila Mkumbo aliyekuwa mjumbe wa CC na Samson Mwigamba aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha – kwa madai ya usaliti, kusingizia viongozi wakuu wa chama na kushirikiana na maadui wa chama.

Akisoma maamuzi ya CC, tarehe 22 Novemba 2013, mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema, Zitto na genge lake wametuhumiwa kwa makosa 11 ya usaliti, yaliyotokana na “Waraka wa Mabadiliko.” Waraka huo ulioandaliwa na Mwigamba na Kitila, ulilenga kuteka chama na kukikabidhi kwa maadui wa chama wakiwamo watu kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).




Zitto ndiye aliandaliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho; naye akakiri kutaka kufanya mapinduzi ya uongozi kinyume na katiba. “…baada ya kumsikiliza Dk. Kitila, Kamati Kuu imebaini kuwa mkakati huo haukulenga kumfanya Zitto kuwa mwenyekiti pekee, bali ulikuwa na malengo makubwa ya kukibomoa chama hicho,” ameeleza Lissu.

Amesema, Zitto alikihujumu chama hicho na kushiriki kujitoa kwa wagombea wake wa ubunge katika majimbo ya Mpanda Mashariki, Musoma Vijijini, Singida Mjini na kuwa mwaka 2006, alipewa magari mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM).

No comments:

Post a Comment