ASEMA WANATUMIA ZAIDINGUVU KULIKO MAARIFA
KUJIRUDIA kwa matukio ya polisi kutumia silaha za moto
dhidi ya raia, kumepokewa kwa hisia tofauti, huku Mwanasheria Mkuu wa Kwanza wa
Serikali, Jaji Mark Bomani akilitaka jeshi hilo kuacha kutumia nguvu wanapokuwa
katika operesheni zao.Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti kuhusu tukio la
hivi karibuni la kupigwa risasi mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania
Daima, watu wa kada mbalimbali walisema, kitendo cha polisi kutumia nguvu sio
busara.
Jaji Bomani kitendo cha polisi kutumia nguvu badala ya
busara katika operesheni zao kinaweza kuleta uhasama kati ya wananchi na jeshi
hilo.
“Kwa ujumla matumizi ya nguvu kwa polisi si mazuri na nadhani tunatakiwa kubadilika katika
hilo.” alisema Jaji Bomani.
Bomani alieleza kuwa
kwa ujumla polisi wanatumia vibaya silaha zao ingawa bado hajapata
uhakika wa jinsi tukio la kujeruhiwa kwa
Matutu lilivyokuwa .
Alisema tukio la Mwangosi lilikuwa baya zaidi lakini
picha anayoiona na kuihusisha na tukio la juzi, ni kuwa kuna matumizi mabaya ya
mashambulizi ya polisi kwa raia.
Hata hivyo wakati Jaji Bomani akieleza hayo Mwenyekiti wa
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji mstaafu Amiri Ramadhan
Manento alisema kila tukio linalofanywa
na polisi linatakiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuanza kulizungumzia.
Jaji Manento alisema akiwa ni mwanasheria hawezi kutoa
hitimisho ya tukio la kujeruhiwa kwa Matutu kabla ya uchunguzi wa kisheria
kufanyika.
“Tunahitaji kujua mambo mengi, ya michakato ya makosa ya
jinai, (criminal procedure) kwa mfano polisi walipoingia walifanya nini,
walipotoka, ni maneno gani walimuuliza mtu wa kwanza waliyekutana naye.
Tunahitaji kujua iwapo walitumia kizuizi cha usalama(safe
cage) katika silaha zao au la” alisema Jaji Manento
Alisema kulingana na taarifa zilizopo katika magazeti
bado unahitajika uchunguzi wa kujua ni
namna gani polisi waliingia ndani ya nyumba hiyo.
Aidha Jaji huyo mstaafu alisema hawezi kuwahukumu polisi
moja kwa moja kwani hakuna ushahidi kuwa walikuwa wakimwinda mwandishi, bali
inawezekana waligundua kuwa ni mwandishi baada ya kumjeruhi.
Alisema hili ni tukio la tofauti na lile la kuuwa kwa
Mwangosi kwani Mwangosi alikuwa kashika vifaa vyake vya kazi lakini hapa Matutu
hakuwa na kitambulisho chochote kuwa ni Mwandishi.
“Unajua polisi wanafuata amri na sheria na wapo kwa ajili
ya kulinda raia wake, hivyo hatuwezi kusema kuwa walikuwa wakimwinda mwandishi,
kwa sababu hata polisi naye amejeruhiwa kwa panga katika tukio hilo,” alisema
Jaji Manento
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dk Kitila Mkumbo
alisema kuwa jeshi la Polisi limekuwa halifanyi kazi zake kwa kufuata weledi
hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya raia kupigwa risasi na Taasisi ya
serikali yenye dhamana ya kuimarisha usalama wa raia hao.
“Matukio haya yanaweza kuathiri amani ya nchi kwa sababu
wananchi wakikosa imani na serikali yao wanaweza kufanya jambo lolote bila
kufuata sharia, matokeo yake amani inatoweka” alisema Dk Mkumbo.
Dk Mkumbo aliongeza kuwa ni vema IGP Saidi Mwema akatilia
mkazo juu ya kufanya kazi kwa weledi ili kuimarisha utendaji kazi wa jeshi la
polisi na kulipa taswira mpya katika jamii.
Mkuu wa Idara ya Fedha waskuli ya Biashara chuoni hapoDk
Esther Ishengoma alisema kuwa jeshi la Polisi linadhamana ya kulinda usalama wa
raia na mali zao, litaendelea kubeba dhamana hiyo, jambo la msingi ni kudhibiti
nidhanu ya askari wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
“Ukiangalia matukio yanayotokea utaona kuna baadhi ya askari
polisi wanaolichafua jeshi kwa kufanya mambo kinyume cha sheria, ni vema suala
la nidhamu likaimarishwa ili kuongeza ufanisi,” alisema Dk Ishengoma.
Mkazi wa Mbagala Mtongani Solomon Isaiah alisema matendo
yanayofanywa na polisi ya kujeruhi na kuua raia
ndani ya kipindi kifupi ni dalili za kutokuwepo utawala bora nchini na
usimamizi mzuri wa ngazi za juu ndani ya Polisi.
“Hawa polisi hawajitakii kufanya hivyo bali wanatekeleza
amri za viongozi wao wa ngazi za juu, hivyo basi lawama, hatua za kisheria na mabadiliko yafanyike kwenye ngazi hizo za
juu za polisi ndipo wahamie kwa polisi wenyewe” alisema Isaiah.
Matukio ya kuua na kujeruhi raia yanayotekelezwa na jeshi
la polisi yamezidi kuongezeka siku hadi siku nchini licha ya wadau na wananchi
kupigia kelele matendo hayo hali ambayo imezidi kugharimu maisha ya Watanzania
wengi wasio na hatia kwa kuchukua sheria mkononi.
Hivi karibuni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
kiliazimia kuishtaki Serikali kwa Mahakama ya Kimataifa ya masuala yaUhalifu(ICC)
ili ichukue hatua zaidi juu ya mfululizo wa matukio ya kutisha yanayofanywa na
jeshi la polisi kwa Wananchi baada ya Serikali kushindwa kuchukua hatua
stahiki.
Kauli hizo imekuja siku moja baada ya polisi
kulizungumzia tukio hilo kwamba lilitokea wakati wakiwa wanajihami.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela
akizungumzia tukio la mwandishi huyo kupigwa risasi alisema alijeruhiwa baada
ya kuanza kumshambulia askari kwa Panga.
Hata hivyo ufafanuzi wa kamanda huyo unatofautiana na ule
wa Matutu na mashuhuda wa tukio hilo, ambao walisema kuwa polisi walivamia
nyumba ya mwandishi huyo iliyopo maeneo ya Kunduchi huku wakimtaka mwanamke
mmoja waliyemtaja kwa jina la mama J.
Katika maelezo yake Matutu alisema polisi hao
walifika nyumbani kwake wakimtaka mkewe baada ya kumfananisha na mtu mwingine,
kwamba wakati akiwa katika harakati za kumtenganisha mke polisi hao baada ya
kuhisi huenda wakawa majambazi ndipo
polisi hao wakampiga risasi ya b
No comments:
Post a Comment