Saturday, December 17

SUALA LA POSHO ZA VIKAO: WAZIRI MKUU-ANAPASWA KUCHUKUA HATUA MBILI, AFUKUZWE AU AJIUZULU! - zittokabwe.wordpress.com

Kwanza nasikitika kuwa Waziri Mkuu amerejesha suala la posho za vikao kwenye mjadala ilhali lilimalizwa baada ya Bungekupitisha Mpango wa maendeleo wa miaka 5. Kitendo cha Waziri Mkuu kulilia posho kinaonyesha jinsi asivyo tayari kusimamia na kutetea sera za serikali anayoongozwa. Anapaswa kuchukua hatua mbili, ama afukuzwe kazi kwa kwenda kinyume na maamuzi ya kisera ya serikali yaliyopitishwa na baraza la mawaziri na Bunge, au ajiuzulu. Hatuwezi kuvumilia viongozi wanaokwenda kinyume na sera za serikali.

No comments:

Post a Comment