Msaanii wa Bongo Muvi,Elizabeth Michael maarufu kama Lulu akiwa na wazazi waki wakiteta jambo na Wakili Peter Kibatala kabla ya shahidi amaye ni Daktari wa Hospitali ya Muhimbili kutoa ushahidiwake mbele ya mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.
Msaanii wa Bongo Muvi,Elizabeth Michael maarufu kama Lulu akipitia maelezo aliyochukuliwa na Polisi kipindi alipokamatwa ambayo aliyatoa kwaajili ya ushahidi kwa kuhusishwa na kifo cha Msanii Mwenzake Steven Kanumba. Maelezo hayo ameyapitia leo katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam.
Msaanii wa Bongo Muvi,Elizabeth Michael maarufu kama Lulu akitoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kusikiliza Shahidi aliyeufanyia uchungunguzi Mwili wa Steven Kanumba.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MAHAKAMA Kuu kanda ya Dae es Salaam leo imeambiwa kuwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba ulikatwa vipande vipande na kupelekwa kwa mkemia kwaajili uchunguz zaidi.
MAHAKAMA Kuu kanda ya Dae es Salaam leo imeambiwa kuwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba ulikatwa vipande vipande na kupelekwa kwa mkemia kwaajili uchunguz zaidi.
Daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya binadamu na vifo vyenye utata kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Inocent Mosha ameeleza hayo mbele ya Jaji Sam Rumanyika wa mahakama hiyo.
Amedai, vipande vilivyopelekwa kwa mkemia ni pamoja na kipande cha utumbo, chakula kilichomo, kipande cha ini, figo, mkojo, damu, mamji maji kwenye jocho na kucha.
Amedai, vipande vilivyopelekwa kwa mkemia ni pamoja na kipande cha utumbo, chakula kilichomo, kipande cha ini, figo, mkojo, damu, mamji maji kwenye jocho na kucha.
Akiongozwa na wakili wa serikali Faraja George shahidi huyo amedai , Aprili 9, 2012 akiwa kazini kwake katika hospitali ya Muhimbili alipokea amri halali ya polisi ikimuamuru kufanya uchunguzi wa Mwili wa Kanumba uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Amedai kuwa wakati wa uchunguzi huo walikuwa na mashahidi wawili walioenda kusaidia kutambua mwili wa marehemu na kuongeza kwenye uchinguzi walianza kuangalia kama ana majera ya nje ya mwili.
Amedai kucha zake za vidole zilionekana kuwa na rangi ya bluu, pia walipofungua viungo vya ndani vya mwili wa marehemu, kwenye sehemu ya kisogo kulikuwa na mvilio wa damu aidha baada ya kufungua fuvu la kichwa ubongo ulikuwa umevimba.
Aliendelea kudai kwenye mishipa midogo iliyokuwemo kwenye ubongo inayosambaza damu ilivilia damu na sehemu ya chini ya ubongo kulikuwa na mkandamizo wa damu
Aliendelea kudai kuwa, alifungua mapafu, moyo, figo, maini, tumbo na mifumo mingine ya mwili haikuwa na tatizo lolote.
Shahidi huyo alidai katika ripoti yake aliyoiandaa kwenda kwa mkemia, ilionesha kuwa anatatizo kwenye mfumo wa upumuaji ambapo ulishindwa kufanya kazi kutokana na majeraha kwenye ubongo.
"Hakuwa na majeraha kwa nje lakini mapafu yalijaa damu ambapo tulikata kucha kufanya vina saba, tulichukua majimaji ya kwenye jicho kuangalia kiasi cha pombe na sukali kwenye mwili" alidai
Pia alidai kuwa pombe haiwezi kusababisha matatizo hayo moja kwa moja badala yake mabadiliko ya tabia yanayotokana na unywaji ndio yanaweza kuchangia.
Alipoulizwa swali na wakili wa utetezi Peter Kibatala shahidi alisema hatambui kama seth Bosco alikuwepo wakati wa uchunguzi kwa sababu sio lazima mtu kuwepo mwanzo mwisho.
Alieleza kuwa hafahamu kiwango cha pombe na hafahamu kama alijigonga kwasababu ya pombe na kwamba hawakuchukua sampuli ya ubongo.
No comments:
Post a Comment