Wednesday, November 15

MAVUNDE AFUNGUA KONGAMANO LA VIONGOZI VIJANA BARANI JIJINI DAR ES SALAAM


 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Viongozi Vijana Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, ambao umehudhuriwa na Vijana zaidi ya 100 kutoka Mataifa mbalimbali ,Kongamano hilo lilikuwa likijadili namna ya fursa zilizopo kwa Vijana katika kutumia rasilimali za nchi zao kama Viongozi katika kujiletea maendeleo
 Mratibu wa kongamano hilo kutoka Taasisi ya The Open Society Initiative for Eastern Africa,Adam Anthony akizungumza kabl ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua kongamano hilo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akiwa meza kuu pamoja na Mratibu wa kongamano hilo kutoka Tasisi ya The Open Society Initiative for Eastern Africa,Adam Anthony na Balozi wa Uholanzi nchini Lianne Houben
 Balozi wa Uholanzi nchini Lianne Houben, akitoa neno kwa vijana kama mfadhili wa kongamano hilo lililowaleta Viongozi Vijana zaidi ya 100 kutoka bara la Afrika
 Msanii wa Muziki wa kughani na mshahiri maarufu barani Afrika , Mrisho Mpoto akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nini Vijana wanatakiwa kufanya ili waweze kuwa Viongozi bora katika Mataifa wanayotoka.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde , akipiga Selfier na Vijana walioshiriki Mkutano huo.


Vijana walioshiriki Mkutano wa Viongozi Vijana Barani Afrika wakifatilia mada mbalimbali zinazoendelea katika kongamano hilo
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera , Bunge , Kazi, Vijana , ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Vijana walioshiriki kongamano la Viongozi Vijana Barani Afrika

Muhubiri awalisha mende wafuasi wake Afrika Kusini

Mhubiri mashuhuri anayetumia nyoka nchini Afrika Kusini Penuel Mnguni amewalisha mende ndugu wawili
Image captionMhubiri mashuhuri anayetumia nyoka nchini Afrika Kusini Penuel Mnguni amewalisha mende ndugu wawili
Muhubiri mashuhuri anayetumia nyoka nchini Afrika Kusini Penuel Mnguni amewalisha mende ndugu wawili katika mkusanyiko wa kanisa lake akidai kwamba wadudu hao walibadilika na kuwa jibini kwa mmoja wao na kiungo kwa mwengine.
Kisa hicho kinajiri takriban miezi mitano baada ya Mnguni katika ibada ilioandaliwa na Muhubiri wa Nigeria TB Joshua, na kukiri kulingana na bwana Joshua kwamba kuwalisha watu haijaandikwa katika biblia.
Kanisa la bwana Mnguni lilichapisha katika mtandao wa facebook kuhusu kisa hicho cha kula mende mapema mwezi huu akisema kuwa muhubiri huyo alimwita mende kuja katika kanisa hilo.
Baadaye aliwaita wafuasi wa kanisa hilo kujitokeza mbele na kula....ndiposa ndugu wawili walijitokeza na kula pamoja...na walipokuwa wakila bwana Charles alihisi anakula jibini huku Bwana Eric akihisi kula kiungo, chapisho hilo lilisema.
Huku akizungumza maneno haya ''uwezo wa mungu uliwagusa wote wawili, kwa kuwa walipo'' , aliongezea.
Kanisa hilo pia liliripoti katika chapisho jingine kwamba muhubiri huyo aliliombea uwa la sumu , na baadaye mfuasi mmoja alilila ua hilo pekee na kulimaliza.
Nabii huyo aliyejitangaza alizua utata nchini Afrika Kusini 2015 baada ya kushutumiwa kwa kuwalisha nyoka wafuasi wake.
Mashtaka dhidi ya Mnguni yaliowasilishwa na shirika la kuzuia ukatili dhidi ya wanyama ,yalitupiliwa mbali mnamo mwezi Julai 2015 kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Auawa kwa kusafirisha ng'ombe India

Wahindu hueshimu sana ng'ombe na ni kosa kubwa kula nyama yake
Image captionWahindu hueshimu sana ng'ombe na ni kosa kubwa kula nyama yake
Viongozi wa kijamii katika mji wa Rajasthan nchini India wanasema mtu mmoja ambaye ni muislam ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaoamini ng'ombe kuwa mungu wao.
Ummar Khan alikua akisafirisha ng'ombe yeye na mwenzake katika kitongoji cha Alwar wakati walipovamiwa na wahindu.
Wanasema kwamba mwili wa kijana huyo ulitupwa karibu na reli kuharibu ushahidi.
Polisi katika mji wa Rajasthan wameanzisha upelelezi juu ya tukio hilo.
Umekuwa ni utamaduni wao tokea enzi na enzi
Image captionUmekuwa ni utamaduni wao tokea enzi na enzi
Wahindu huamini kuwa ng'ombe ni mungu kwao na huwachukulia kwa namna ya upekee sana.
Zaidi ya watu kumi wameuawa tokea mwaka 2015 kwa sababu kama hizo.

Davido ampiku Wizkid kushinda tuzo ya MTV

Nyota wa muziki nchini Nigeria Davido
Image captionNyota wa muziki nchini Nigeria Davido
Nyota wa Nigeria Davido amempiku Wizkid na kushinda tuzo la muziki za Ulaya MTV na kutuzwa kama mwanamuzik bora wa Afrika.
Davido na Wizkid wameteuliwa kwa tuzo hizo mara mbili wakiwa pamoja.
Davido alikuwa akiwatumbuiza mashabiki wake katika mji mkuu wa Luanda nchini Angola wikendi hii kwa hivyobasi hakuweza kupata fursa ya kushiriki tamasha hiyo.
Lakini amewashukuru kila mmoja ikiwemo mamake kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa picha wa Instagram:
Kwenye chapisho lililosema niko FiAAAAAAA!!! Akizungumzia wimbo wake mpya wa FIA:
Washindani wenzake walioteuliwa katika tuzo hizo ni pamoja na Nasty C na Babes Wodumo kutoka Africa Kusini, Nyashinski kutoka Kenya na C4 Pedro wa Angola.
Hivi majuzi aliiambia kipindi cha radio cha BBC Focus on Africa kabla ya tamasha hiyo , kwamba ilikuwa ni wakati kwa raia kutoka Ureno kushinda tuzo hiyo.

Sweden yaipa Tanzania msaada ya Sh 400 bilioni

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James 
Dar es Salaam.Sweden imeipatia Tanzania msaada wa Sh435 bilioni ili kuchangia katika bajeti ya Serikali na kuiwezesha sekta ya elimu.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini leo Jumanne kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini, Ulf Kallstig.
“Naomba ieleweke kwamba huu sio mkopo ni msaada, hatutakiwi kuurudisha,” amesema katibu mkuu baada ya kusaini mikataba mitatu.
Akifafanua, amesema kati ya kiasi hicho Sh159.4 bilioni zimetolewa na nchi hiyo ili kuisadia Serikali kuchangia kwenye bajeti yake ya 2017/18 hadi 2018/20.
Amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani yanayohusu kodi na yasiyo ya kikodi.
Katika mkataba wa pili, Dotto amesema Sweden ameipatia Serikali Sh235.39 bilioni ili kusaidia elimu kwa kufuata vipaumbele vilivyopo.
“Unajua tangu Serikali imeanza kutoa elimu bure imekuwa ikitenga bajeti kubwa katika elimu kushinda sekta nyingine ndiyo maana marafiki zetu wameamua kutusaidia,”amesema.
Amesema sekta ya elimu imekuwa ikitengewa asilimia 18 ya bajeti yote ya Serikali na kuifanya sekta hiyo kuongoza kwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.
Jamese amesema katika mkataba wa tatu, Sweden imetoa Sh40.72 bilioni ili kuongeza katika mradi wa kuwaelimisha watoto waliokosa elimu ya msingi kwa sababu ya matatizo mbalimbali.
Amesema Sweden imekuwa ikisaidia fedha kwa ajili ya kuwapa elimu watu wa aina hiyo tangu mwaka 2015 hivyo imeamua kuongeza fedha.
“Msaada huu unaonyesha namna nchi hizi mbili zilivyo na ushirikiano,” amesema.
Amesema mbali na msaada huo, Sweden imekuwa ikiisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo za nishati na uwezeshaji katika tafiti.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo Ubalozi wa Sweden nchini, Kallstig amesema elimu ndiyo msingi wa maendeleo katika nchi zote.
Amesema ndiyo maana nchi hiyo imekuwa ikisaidia sekta ya elimu na inafurahishwa na mageuzi ya elimu yanayofanyika hapa nchini.

Ripoti inayoeleza unyanyasaji wa Watanzania Uarabuni ilivyozuiwa Dar

Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Human Rights
Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Human Rights Watch, Audrey Wabwire akiwaonyesha wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kitabu kilicho na Ripoti inayoangazia watumishi wa ndani kutoka Tanzania wanaopelekwa nchini Oman . Picha na Omar Fungo 

Dar es Salaam. Maofisa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) wamezuia kuzinduliwa kwa ripoti ya unyanyasaji wa watumishi wa ndani wa Kitanzania nchini Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Ripoti hiyo inatokana na utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu (Human Rights Watch) ilitakiwa kuzinduliwa saa nne asubuhi jana katika ukumbi wa Holiday Inn.
Hata hivyo kabla ya kuzuiwa ripoti hiyo ilikuwa imeshasambazwa kwa waandishi wa habari.
Ofisa mtafiti wa Costech, Dk William Kindeketa alisema walilazimika kuzuia ripoti hiyo kwa sababu watafiti hawakufuata taratibu zinazotakiwa.
“Kwetu sisi utafiti wowote ule unaofanyika uwe wa kijamii au kisayansi, Costech ndio wenye mamlaka ya kupitisha,” alisema.
Dk Kindeketa alisema taratibu hizo ni kuandika dokezo, kujaza fomu na wasifu wa taasisi au shirika linalotaka kufanya utafiti.
Maofisa hao ambao baadaye waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa wamefika kwa ajili ya uzinduzi wa ripoti hiyo, walisema hadi watafiti hao watakapotimiza masharti yote ndipo wataruhusiwa kutoa ripoti.
Akiahirisha uzinduzi huo, ofisa mawasiliano wa Human Rights Watch, Audrey Wabwire alisema maofisa hao walifika tangu saa tatu asubuhi kwenye eneo la mkutano wa waandishi wa habari, wakafanya nao kikao lakini baadaye wakazuia kuzinduliwa kwa ripoti hiyo.
Kulikuwa na mvutano ambapo awali maofisa hao walizuia waandishi kuingia ukumbini lakini baadaye wanahabari waliruhusiwa kuingia huku wao wakitoka kabla ya kuzuia na kuwaondoa.
Katika ripoti hiyo ambayo tayari ilikuwa imeshasambazwa ilieleza kuwa watumishi wa Kitanzania wanaofanya kazi katika nchi hizo wanatimiza majukumu yao kwa saa nyingi za kazi, kutolipwa mishahara, ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kimwili kinyume na haki za binadamu.
Katika ripoti hiyo yenye kurasa 99 iliyoandikwa ‘Kufanya kazi mithili ya roboti’, pia imeweka kumbukumbu ya namna watumishi hao wanavyonyanyasika na kutolipwa.
Mtafiti wa haki za wanawake Mashariki ya Kati wa Human Rights Watch katika ripoti hiyo, Rothna Begum amesema kwenye ripoti yake kuwa maelfu ya watumishi wa ndani wa Kitanzania wako Mashariki ya Kati. “Human Rights Watch ilifanya mahojiano na watu 87 ikiwa ni pamoja na maofisa wa Tanzania, vyama vya wafanyakazi, mawakala wa uajiri, watumishi wa ndani wanawake 50 wa Kitanzania ambao walifanya kazi Oman na UAE,” amesema. Ripoti hiyo imesema baadhi ya wahanga walidai kufanyishwa kazi kwa saa 21 kwa siku bila mapumziko, kula chakula kilichoharibika na wengine kunyanyaswa kimwili ikiwamo kulazimishwa kufanya ngono na kubakwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wote waliohojiwa walisema waajiri wao walitaifisha hati zao za kusafiria na kujikuta wakiwa na njia finyu za kujinasua na ukatili huo.
“Baadhi ya matukio haya ni sawa na kazi za shuruti au biashara haramu ya kusafirisha binadamu,” imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imeishauri Tanzania kuwa na mikakati maalumu ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa watumishi hao ikiwa ni pamoja na kuandaliwa kwa kanuni kali zitakazoongoza ajira zao.
Pia, watafiti katika ripoti hiyo wanashauri kuwapo kwa programu za mafunzo ya haki na msaada wa kujitosheleza kutoka katika balozi za Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwalipia gharama za tiketi za kurudi nyumbani wafanyakazi hao inapotokea unyanyasaji.
“Tanzania inapaswa kuhakikisha kwamba wanawake wanaweza kuhama kwa usalama kwa ajili ya kazi za ndani. Oman na UAE lazima zifanye kazi pamoja kuzuia unyonyaji wa watumishi wa ndani wahamiaji, kuchunguza unyanyasaji na kuwashtaki wale wanaohusika,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Kampeni meneja wa CCM adaiwa kushambuliwa na wafuasi wa Chadema


Mwanza. Kampeni meneja wa mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM Kata ya Mhandu jijini Mwanza, Joseph Warioba amevamiwa na kucharangwa mapanga sehemu ya kisogoni na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema jana Jumanne jioni.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Fustine Shilogile amekiri kutokea kwa tukio hilo na tayari watu wawili wameshatiwa mbaroni kwa kuhusika na tukio hilo.
Alisema kundi hilo ambalo halijafahamika idadi yake lakini lilikuwa likitoka kwenye kampeni za uchaguzi wa Chadema zilizokuwa zinafanyika katika Uwanja  wa Shule ya Msingi Nyakato ndipo waliposhuka wakiwa na mapanga na kuanza kumshambulia.
“Tayari tumefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao majeruhi aliwatambua na tunaendelea kuwahoji ili wawataje na wengine waliohusika kwenye tukio hilo,”
Shilogile alisema wanaendelea kufuatilia kampeni zote zinazofanyika na kuhakikisha zinakuwa za amani na watakaoenda kinyume watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumzia tukio hilo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala alisema Warioba alivamiwa jana na kundi la watu zaidi ya sita ambao walishuka kwenye gari aina ya Noah eneo la viwandani Nyakato kisha kuanza kumshambulia kwa mawe mapanga na visu.
Warioba ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ulinzi wa Chadema Kanda ya Ziwa alikihama chama hicho na kuhamia CCM ambapo amekuwa akimnadai mgombea udiwani wa CCM, Constatine Sima katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.
 “Ni kweli kampeni meneja huyo alivamiwa na kundi kubwa la vijana ambao ni wafuasi wa Chadema na kuanza kumshambulia kwa mapanga, taarifa tumeshaziripoti polisi kituo cha Nyakato,” alisema Mangwala na kuongeza
“Kutokana na kupata majeraha makubwa alipelekwa hospitali ya Buzuruga kwa ajili ya matibabu,”
Mwagwala alisema walichokifanya wapinzani sio kizuri huku akiwataka kuendesha kampeni kwa hoja ili kumpata mshindi atakayekuwa msaada kwa jamii.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Warioba alisema wote waliomshambulia anawafahamu na kwamba atakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

Kwa udhalilishaji huu wa watoto Zanzibar, hapana


Karibu kila siku jua linapochomoza kuanza safari yake ya kutoka Mashariki kwenda Magharibi ukifungua redio, ukiangalia runinga au ukisoma habari za magazeti na mitandaoni hadithi kubwa ni moja tu.
Nayo ni ya unyanyasaji, ubakaji, unyama na ujahili usioelezeka wanaofanyiwa watoto, unaokithiri kwa kasi katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Hata kuviita vitendo hivi ni unyama bado hujavipa maelezo yanayostahiki kwa sababu hata wanyama wakubwa na wakali huonyesha huruma na imani kwa wanyama wadogo.
Kwa mfano sijaona au kusikia katika umri wangu pandikizi la jogoo kumbaka kifaranga. Kubwa zaidi hata anapotaka kufurahisha mahitaji yake ya kimwili kwa kuku mwenye vifaranga jogoo huondoka shingo upande likitunisha mbawa kuonyesha kwamba koo huyo bado analea.
Lakini baada ya balaa la kusambaratisha mikutano ya wanaume wanaodaiwa kushabikia kuingiliana kimwili kati yao, pamezuka wimbi kubwa na lenye dhoruba la vijana na hata wazee kuwafanyia uchafu usioelezeka watoto wadogo wa kike na kiume.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba miongoni mwa wanaofanya huu udhalilishaji unaoweza kusema ni laana, ni wazee na wana wa familia na ungetarajia hivi vitoto kukimbilia kwao na kukumbatiwa kwa upendo. Lakini loo, salaale … huko ndiko unakoweza kusema kukimbia kuungua ndani ya kikaango na kutumbukia kwenye moto mkali wa vifuu vya nazi.
Maskini watoto wetu, wamegeuzwa mayatima wasiokuwa na walezi wa kuwategemea pale wanapopata shida.
Katika orodha ndefu ya matokeo zaidi ya 10 katika wiki moja iliyopita Unguja na Pemba, watu wazima zaidi ya miaka 50 na wengine wenye familia wamewanajisi watoto wadogo waliokuwa kwa raha na furaha wakiwaita babu.
Hapo mwanzo uchafu huu ulionekana kukithiri mijini, lakini sasa umetapakaa hata vijijini. Kwa mfano kule Pemba, katika Kijiji cha Kiungoni yupo mzee mmoja anayedaiwa kuwabaka watoto wake watatu wa kambo.
Maskini mama mzazi wa watoto hawa. Alipopata mume alitegemea kumsaidia kulea vitoto vyake kumbe kaingia katika tanuri la kumharibia wanawe.
Alipoolewa huyu mama aliona kama kaondokana na joto la karai liliokuwa jikoni liliokuwa na maisha magumu, lakini kumbe ametumbukia kwenye tanuri la moto la kumharibia wanawe.
Katika Kijiji cha Mkokotoni, Kaskazini Unguja, zimesikika taarifa za mtoto wa kiume wa miaka mitano kubakwa na kwenda kufanyiwa uchafu usioelezeka na kurudishwa nyumbani kwao alfajiri akiwa ameharibiwa vibaya sana.
Kwa tukio hili la Mkokotoni tunaambiwa hayo yamefanywa na hao ambao siku hizi wamepewa jina la watu wasiojulikana.
Hapa yanazuka maswala mengi, kama nini hasa kilichosababisha kuwepo hali hii mbaya Visiwani?
Mengine ni wanaofanya haya wanapata raha gani, nini lengo lao, nini kinafanyika kudhibiti hali hii na hatua gani zinafaa kuchukuliwa haraka kupunguza maafa zaidi siku za usoni.
Kwa kweli yapo mengi yanayolizunguka suala hili, kama ngoma ya mduara ambapo mchezaji kila akizunguka anajikuta anarudi palepale alipoanzia.
Lakini hii haina maana kuachia huu mzunguko kuendelea, lazima ukatwe kwa sababu si mzunguko wa kheri na hauna manufaa kwa Zanzibar na watu wake.
Kwanza ni vyema kukubali bila ya kutafuna ulimi au kupepesa macho kuwa maadili yameporomoka sana Visiwani na yanahitaji ukarabati mkubwa, kama si ujenzi mpya.
Hii litawezekana kwa kuongeza elimu ya kidini na dunia kwa jamii ili watu wawe na uelewa mpana wa suala hili lilivyo na athari zake za hivi sasa na baadaye.
Ni kwa kuwa na jamii yenye uelewa ndio itawezekana kupiga hatua moja mbele. Nayo ni kila mtu kuwa mchungaji wa haki za mtoto, kuachana na ukimya juu ya suala hili, kuondoa muhali kwa wanaotenda na kushabikia kwa ati mhusika ni ndugu, jamaa au rafiki yangu au kwa miaka mingi tumeishi vizuri na wazee wake.
Hapahapa suala la huruma, wema wala hisani bali haki. Hata siku moja haki haiwezi kufunikwa na kawa la wema na hisani. Haki lazima itafutwe na ipatikane kwa gharama yoyote ile.
Elimu pia iongezwe katika shule na madrasa ili watoto wawe na uelewa mzuri wa kuwepo janga hili na wajue njia za kujikinga na wafanye nini anapotokea mshenzi anayetaka kuharibu maisha yao.
Katika nchi nyingi za wenzetu hili inafanyika na
imepata mafanikio. ujifunze kutokana na uzefu wao.
Vyombo vyetu vinavyosimamia sheria, yaani polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na mahakama nazo ziongeze kasi ya zionekane zinajitahidi kuhakikisha wakati wote haki inatendeka.
Wachache miongoni mwetu waliomo katika taasisi hizi ambao wanatiliwa mashaka ya kukosa uadilifu wawekwe kando ili wenye nia njema ya kunusuru maisha ya watoto wapate nafasi ya kusonga mbele. Lakini pia sheria zilizopo zimulikwe na kuangaliwa kama zinakidhi haja ya kuikabili hali hii.
Kwa muda mrefu kuna malalamiko juu yakesi hizi kuchukua muda mrefu na hata mashahidi kuchoka na nenda rudi mahakamani ya kesi kuahirishwa. Suala la posho ya usafiri kwa mashahidi nalo litupiwe jicho la huruma.     

Rais Mugabe ajiandaa kujiuzulu


Harare, Zimbabwe. Taarifa za hivi punde kutoka vyanzo vya ngazi ya juu ni kwamba Rais Robert Mugabe “anajiandaa kujiuzulu” baada ya usiku uliotawaliwa na mlio wa risasi na makazi yake kuzingirwa na jeshi.
Hakuna maelezo zaidi isipokuwa Jeshi limesema asubuhi leo kwamba Rais Mugabe na mkewe Grace wamehifadhiwa mahali na kwamba linalinda usalama wa ofisi za serikali na linafanya doria kwenye mitaa mbalimbali baada ya usiku wa ghasia uliohusu kuzingirwa kwa majengo ya shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC).
Matukio ya usiku kucha yamesababisha watu kuvumisha kwamba yamefanyika mapinduzi huku wanaounga mkono hatua hiyo wakisifu kwamba ni “marekebisho yasiyo ya umwagaji damu.”
Askari wenye silaha wakiwa kwenye magari yao walijipanga kwenye maeneo muhimu katika jiji la Harare na asubuhi Wazimbabwe walionekana kwenye mistari mirefu kwenye mabenki kwa lengo la kuchukua fedha utaratibu ambao hutokea mara nyingine kunapotokea mgogoro wa kifedha.
Wengine walionekana wakitazama simu zao kusoma habari juu ya jeshi kunyakua madaraka huku wengine wakienda kazini.
Katika hotuba iliyorushwa asubuhi baada ya kudhibiti shirika la utangazaji, msemaji wa jeshi alisema jeshi limewalenga “wahalifu” wanaomzunguka Mugabe na liliwahakikishia raia kwamba utulivu utaimarishwa.
Shauku ya kujua alipo Mugabe, 93, na mkewe ilikuwa kubwa lakini inaelekea wamewekwa chini ya kizuizi cha jeshi. "Usalama wao ni wa uhakika," amesema msemaji wa jeshi.
"Tunapenda kuweka wazi kuwa jeshi halijatwa madaraka,” alisema msemaji wa jeshi. "Sisi tunawalenga wahalifu wanaomzunguka (Mugabe) ambao wanafanya uhalifu na kusababisha mateso ya watu kijamii na kiuchumi nchini na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria."

Lulu akubali kukaa jela


Imeelezwa kuwa baada ya msanii  Elizabeth Michael kusomewa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela, aliwaambia ndugu zake wasikate rufaa kwa kuwa kilichotokea ni mipango ya Mungu na yupo tayari kukabiliana nayo.
Msanii , Muhsin Awadh maarufu Dk Cheni ambaye amekuwa karibu na mwigizaji huyo katika kipindi chote amesimulia hali ilivyokuwa  muda mfupi  baada ya jaji kutoa hukumu hiyo.
“Kusema ukweli Lulu alijua lolote linaweza kutokea ila la kufungwa ni kama hakulipa kipaumbele sana, jaji alipomaliza kusoma hukumu alishtuka kama sisi wengine wote lakini ajabu alikuwa wa kwanza kurudi katika hali ya kawaida na kutoa kauli za ujasiri,” anasimulia Dk Cheni
 Lulu alisema: "Sipingani na maamuzi ya Mungu, haya ni maamuzi yake na nimekubaliana nayo. Ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo".
Anasema kingine alichowaambia ni kuachana na masuala ya kukata rufaa kwa sababu bado hatakuwa huru: "Acheni miaka miwili siyo mingi, sitaki kupingana na mahakama , naheshimu maamuzi ya mahakama, acheni nitumikie kifungo changu. "
Mapema wiki hii mwigizaji huyo alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji mwenzake Steven Kanumba, Aprili 7,201

Bob Wangwe ahukumia kulipa faini au jela mwaka mmoja



Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Bob Wangwe ambaye ni mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, kulipa faini ya Sh 5 milioni ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.
Bob ana taaluma ya sheria na mwanaharakati wa haki za binadamu.
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ametoa hukumu hiyo leo Jumatano baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa  upande wa mashtaka, vielelezo vitano na utetezi wa mshtakiwa mwenyewe.
Amesema kuwa Mei 7, 2016 askari polisi walipata taarifa ya chapisho la mtoto huyo wa Chacha Wangwe, na walianza kumfuatilia na kumkamata kisha walichukua simu na kuipeleka maabara ya polisi ili kuikagua.
Bob hukupinga kuandika maneno hayo lakini alidai kuwa hakuyachapisha katika mtandao wa kijamii bali yalikuwa ni siri kwenye akaunti yake.
Hakimu Shaidi amesema wakati wa ushahidi imeelezwa kuwa simu yake ilipokaguliwa ilionekana ilitumika kuchapisha ujumbe huo kwa jamii na watu walijibu, ikiashiria ujumbe uliwafikia.
“Nidhahiri ulikuwa na nia ya kuchapisha taarifa hiyo, kueleza kile ambacho ulikiona sahihi kama ingekuwa ni ujumbe wako binafsi basi polisi wasingeweza kukutafuta na watu wasingekujibu.” 
Hakimu Shahidi amesema kutokana na hatua hiyo Bob amekutwa  na hatia chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015.
Bob ameomba apunguziwe adhabu kwa sababu ni mwanafunzi wa masomo ya sheria, pia ni kijana mdogo na ni kosa lake la kwanza kulitenda.
Hakimu Shaidi amesema anakubaliana na hoja za Bob, kwani Mahakama inamuona bado ni mdogo na anapaswa kufanya mambo mengi mazuri katika jamii.
Pia amesema kama yeye ni mwanafunzi wa masomo ya sheria anapaswa kufanya mambo mema katika jamii vitu ambavyo wengine watamuiga.
Mahakama imemhukumu kulipa faini ya Sh 5 milioni ama kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela. Hata hivyo alifanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kukwepa kifungo.
Katika kesi hiyo namba 167, 2016 Bob alikuwa anakabiliwa na shtaka la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

Sheria ya matumizi ya ramani yaja


Dodoma. Serikali imewasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2017, ambapo moja ya marekebisho hayo ni kuweka faini ya hadi Sh10 milioni kwa atakayesambaza ramani potofu.
Akiwasilisha muswada huo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amesema adhabu kwa kosa hilo itakuwa faini isiyopungua Sh5 milioni lakini isiyozidi Sh10 milioni.
Endapo atashindwa kulipa faini hiyo, atalazimika kutumikia kifungo kisichopungua miezi sita lakini kisichozidi miaka miwili.
Masaju amesema lengo la marekebisho ya kifungu hicho kinachohusu upimaji na ramani ni kudhibiti ramani zinazopotosha mipaka sahihi ya maeneo.
Marekebisho hayo yana lengo la kumpatia mkurugenzi wa upimaji na ramani haki ya kipekee ya kuandaa, kutengeneza na kusambaza ramani zote zinazoonyesha mipaka ya mikoa na nchi.

Jeshi Zimbabwe lawatia ndani mawaziri watatu


Harare, Zimbabwe. Mawaziri kadhaa katika serikali ya Rais Robert Mugabe wamekamatwa baada ya Jeshi la Ulinzi kuonyesha uwezo wake na kushikilia majengo yakiwemo ya shirika la utangazaji (ZBC).
Milipuko mikubwa ilisikika na ikafuatiwa na ya bunduki katika maeneo yanayokaliwa na watu maarufu ya Borrowdale usiku kucha hali iliyozidisha hofu kwamba jeshi lilikuwa kazini.
Shirika la TimesLIVE limeripoti kwamba waliokamatwa ni watu maarufu kutoka kundi la G40 ndani ya chama cha Zanu PF lililokuwa likiongozwa na memsapu wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.
Baadhi ya watu waliokamatwa ni Waziri wa Elimu Jonathan Moyo‚ Serikali za Mitaa Saviour Kasukuwere na Waziri wa Fedha Ignatius Chombo.
Jeshi limesema katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake moja kwa moja kupitia ZBC kwamba Rais Mugabe yuko “salama na mwenye afya njema”. Taarifa hii imekuja baada ya askari wakiwa na silaha jana Jumanne kwenda katikati ya mji wakiwa kwenye magari ya kijeshi.
Shirika la Utangazaji la Zimbabwe ambalo majengo yake yako eneo la Pocket Hills jijini Harare lilitekwa saa 10:00 alfajiri.
Msemaji wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alitangaza kwamba jeshi lilikuwa linadhibiti kwa lengo la kuhakikisha linawashughulikia “wahalifu” wanaomzunguka Mugabe.
“Sisi tunawalenga wahalifu wanaomzunguka yeye (Mugabe) wanaofanya uhalifu ambao unawasababishia watu mateso katika Nyanja za kijamii na kiuchumi hapa nchini na kisha tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria‚” alisema Moyo.

Dk Shika atimiza ahadi ya polisi


Dar es Salaam. 'Bilionea' Dk Louis Shika aliyeibuka mshindi wa kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi leo Novemba 15  ameripoti kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam kama alivyotakiwa.
Dk Shika ameripoti kama alivyotakiwa jana na Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa mara baada ya kuachiwa kwa kujidhamini yeye mwenyewe.
Kabla ya kwenda kuripoti, Dk Shika ambaye amekuwa maarufu kila anapopita, alipata kifungua kinywa maeneo ya Posta.
Saa 2.24 asubuhi, Dk Shika alikuwa amewasili kituoni hapo na ilipofika Saa 3.36 asubuhi aliondoka na kesho atarejea tena kituoni hapo.
Akizungumza na Mwananchi lililokuwapo tangu anaingia hadi anatoka amesema hana tatizo na ataendelea kuitikia wito wa polisi bila tatizo.

Meneja wa Diamond asema hana uwezo wa kulipa Sh 250 milioni


Dar es Salaam. Wakati siku 14 zilizotolewa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart & Co Ltd, kwa wakurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection Limited kutekeleza amri ya Mahakama zikikaribia kuisha, Hamis Taletale (Babu Tale), amejitetea huku akidai kuwa anajiandaa kisaikolojia kwa kifungo.
Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnum, pamoja na nduguye Iddy Taletale ni wakurugenzi na pia wanahisa wa kampuni hiyo.
Februari 18, 2016, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliiamuru kampuni hiyo kumlipa fidia ya Sh250 milioni Mhadhiri wa Dini ya Kiislam Sheikh Hashim Mbonde, kwa kutumia kibiashara mahubiri yake bila ridhaa wala makubaliano.
Babu Tale amekiri kupokea taarifa hiyo ya Yono, lakini akasema kuwa yeye hajui chochote kuhusu madai hayo, kwani hakuwahi kujihusisha  na kampuni hiyo na kwamba hana cha kufanya bali anawasubiri kuona Yono hizo siku walizopewa ili waone hatua zitakazofuata. 
“Lakini mimi nasema sijamdhulumu huyo mzee wala sijawahi kufanya naye biashara. Kwa kuwa hiyo ni amri ya Mahakama sawa sina cha kufanya, kama watasema tulipe nitaeleza uwezo wangu maana mimi sina uwezo huo wa kulipa hizo Sh250 milioni,” amesema na kuongeza:
“Kwa hiyo cha kufanya ni kujiandaa tu kisaikolojai hata kama ni kufungwa, kwani hata kina Mandela (Nelson) walifungwa jela hivyo hivyo.”
Amesema kuwa kampuni hiyo ilifunguliwa na ilikuwa ikimilikiwa na kaka yao Abdul Taletale (marehemu kwa sasa) kwa asilimia miamoja na kwamba baada ya kufariki kampuni hiyo haikuendelea na mali zake zote zilipotea kwani zilidhulumiwa.
Amesema kuwa japo anatajwa kama mhusika lakini hakuwahi kuwa mkurugenzi, mwanahisa wala kujihusisha kwa namna yoyote na kampuni hiyo na kwamba  hakuona taabu kwani hakujua kama kuna siku yatatokea matatizo kama haya.  
Ameongeza kuwa alifahamu kuwepo kwa kesi hiyo baada ya kaka yao kufariki, ambapo wakili wa mdai alimpigia simu akimtaka afike mahakamani, lakini yeye alipuuza kwa kuwa alijua si mhusika.
Kwa mujibu wa hukumu ya kesi ya msingi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, Juni 6, 2013 Sheik Mbonde aliingia makubaliano na kampuni hiyo, kutumia kazi zake za mawaidha, kwa kuzalisha, kurekodi na kuzisambaza na kugawana faida ya mauzo.
Hata hivyo, baada ya kukamilisha kurekodi masomo saba, kampuni hiyo ilimkatia mawasiliano hadi alipobahatika kukutana na ofisa mmoja wa kampuni hiyo,  Adam Waziri ambaye alimweleza kuwa wamesitisha mpango huo.
Lakini Agosti 9, 2013, wakati mdai akiendesha mhadhara Bahi Dodoma, alibaini kuwa DVD za masomo yake zilikuwa zikiuzwa sokoni Dodoma na katika  mikoa mbalimbali, bila ridhaa yake wala makubalino ndipo akafungua kesi hiyo.