Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Fustine Shilogile amekiri kutokea kwa tukio hilo na tayari watu wawili wameshatiwa mbaroni kwa kuhusika na tukio hilo.
Alisema kundi hilo ambalo halijafahamika idadi yake lakini lilikuwa likitoka kwenye kampeni za uchaguzi wa Chadema zilizokuwa zinafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyakato ndipo waliposhuka wakiwa na mapanga na kuanza kumshambulia.
“Tayari tumefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao majeruhi aliwatambua na tunaendelea kuwahoji ili wawataje na wengine waliohusika kwenye tukio hilo,”
Shilogile alisema wanaendelea kufuatilia kampeni zote zinazofanyika na kuhakikisha zinakuwa za amani na watakaoenda kinyume watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumzia tukio hilo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala alisema Warioba alivamiwa jana na kundi la watu zaidi ya sita ambao walishuka kwenye gari aina ya Noah eneo la viwandani Nyakato kisha kuanza kumshambulia kwa mawe mapanga na visu.
Warioba ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ulinzi wa Chadema Kanda ya Ziwa alikihama chama hicho na kuhamia CCM ambapo amekuwa akimnadai mgombea udiwani wa CCM, Constatine Sima katika uchaguzi mdogo wa madiwani unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 mwaka huu.
“Ni kweli kampeni meneja huyo alivamiwa na kundi kubwa la vijana ambao ni wafuasi wa Chadema na kuanza kumshambulia kwa mapanga, taarifa tumeshaziripoti polisi kituo cha Nyakato,” alisema Mangwala na kuongeza
“Kutokana na kupata majeraha makubwa alipelekwa hospitali ya Buzuruga kwa ajili ya matibabu,”
Mwagwala alisema walichokifanya wapinzani sio kizuri huku akiwataka kuendesha kampeni kwa hoja ili kumpata mshindi atakayekuwa msaada kwa jamii.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Warioba alisema wote waliomshambulia anawafahamu na kwamba atakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.
No comments:
Post a Comment