Tuesday, October 31

Nape Nnauye afunguka kuhusu hili

 Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kuweka sawa kuwa siku ya kesho Oktoba 31, 2017 hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya habari na kusema kuwa watu wanatunga hizo taarifa.

Nape Nnauye ametoa kauli hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii na kuwataka watu waache kumzushia mambo wakiwa na lengo la kutafuta nafasi na vyeo serikalini.

"Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina 'press conference' kesho" aliandika Nape Nnauye

Leo mchana watu wasio na nia nzuri na Nape Nnauye walizusha taarifa kuwa kiongozi huyo siku ya kesho Jumanne atakuwa na mkutano na waandishi wa habari jambo ambalo yeye mwenyewe amelipinga na kusema watu wanazusha taarifa hizo kwa maslahi yao wenyewe.

Mwanasiasa wa upinzani ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela Cameroon

Mwanasiasa wa upinzani ahukumiwa miaka 25 jela Cameroon
Image captionMwanasiasa wa upinzani ahukumiwa miaka 25 jela Cameroon
Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limeikosoa mahakama ya kijeshi nchini Cameroon kwa kumhukumu kiongozi mmoja wa upinzani miaka 25 jela kwa makosa ya kuchochea uasi.
Aboubakar Siddiki - kiongozi wa chama cha upinzani kaskazini mwa nchi, ndiye mwanasiasa aliyepelekwa jela katika harakati za Cameroon za kuuzima upinzani hivi karibuni.
Hakuna ushahidi uliotolewa mahakamani kuchangia hukumu kama hiyo , taarifa ya Amnesty International ilisema.
Alikamatwa mwaka 2014 baada ya kulaumiwa kwa kupanga kuipindua serikali ya Rais Paul Biya.
Bwana Biya amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na wakosoaji wake wanamtaja kuwa dikteta.
Watu kadhaa wameuawa na mamia kukamatwa wakati wa maandamano katika eneo hilo lenye watu wanaozungumza lugha ya Kiingereza na ambao wanalalamika kutengwa.

Makonda amjibu Nyalandu

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewata wanasiasa  kukubaliana na hali ya mabadiliko kwani sasa ni muda wa kufanya kazi na sio wakati wa kutafuta umaarufu na maneno mengi.

Macho yote kwa Odinga


Nairobi, Kenya. Kenya imekuwa ikisubiri kwa shauku kubwa siku ya Jumanne ambayo kiongozi wa upinzani Raila Odinga amejiandaa kutoa hotuba juu ya mikakati waliyonayo baada ya kususia uchaguzi wa marudio uliomwezesha Rais Uhuru Kenyetta kupata ushindi wa kishindo.
Kenyatta alitangazwa jana kuwa mshindi wa uchaguzi huo wa Alhamisi kwa asilimia 98 ya kura zilizopigwa matokeo yanayothibitisha hata uchaguzi wa awali wa Agosti 8 alikuwa ameshinda japo yalibatilishwa na Mahakama ya Juu.
Hata hivyo ushindi wa Kenyatta una utamu wenye uchungu. Idadi ya asilimia 38.8 ya watu waliojitokeza inatarajiwa kuibua maswali juu ya kuaminika kwa uchaguzi huo ulioigawa nchi katika pande mbili na kuchochea mapambano ya kisheria na maandamano ya ghasia yaliyodumua miezi kadhaa.
"Kilichofanyika hapa si kingine bali kuhalalisha matakwa ya wapigakura,” alisema Kenyatta katika hotuba yake ya kupokea ushindi huku akikiri uwezekano wa matokeo hayo kukumbwa na changamoto za kisheria.
Upigaji kura wa Alhamisi ulijaa matatizo kama vituo kuzuiwa kutokana na vurugu kwenye kaunti nne  za Nyanza zilizofanywa na wafuasi wa Odinga waliosusia na kusababisha siku mbili za mapambano na vikosi vya usalama. Watu tisa waliuawa.
Hadi jana, Odinga alikuwa kimya lakini amewaahidi wafuasi wake atatoa tam

Zitto ahamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi


Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameanza kuzungushwa katika vituo vya Polisi jijini Dar es Salaam.
Zitto baada ya kuhojiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe mkoani Temeke sasa amehamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema baada ya Zitto kuhojiwa kuhusu aliyozungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za udiwani zilizofanyika Kijichi Jumapili Oktoba 29,2017 aliachiwa kwa dhamana.
Shaibu amesema Zitto aliyewakilishwa na wanasheria Venance Msebo na Steven Mwakibolwa alidhaminiwa na watu wawili na alitakiwa kurudi kituoni hapo Jumatatu Novemba 6,2017. Hata hivyo, amesema alikamatwa tena.
Akizungumzia kukamatwa kwa Zitto, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameieleza Mwananchi kuwa wanamshikilia kwa lugha za uchochezi.
"Tunamshikilia kwa uchochezi na kutoa lugha zisizo na staha na yupo Central hapa,'' amesema Kamanda Mambosasa

Tarime kutoa shukrani kwa Mungu kwa ajili ya Lissu


Tarime. Chadema wilayani Tarime imechangisha Sh3.1 milioni kwa ajili ya matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu, ikisema imeuona mkono wa Mungu kupitia kwake.
Chama hicho kimesema kupitia hilo, wanachama watapita kwenye makanisa na misikiti kutoa shukrani kwa Mungu.
Mbunge huyo anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi katika makazi yake eneo la Area D mjini Dodoma Septemba 7,2017.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche akizungumza leo Jumanne Oktoba 31,2017 wakati wa kuchangisha fedha hizo amesema chama hicho hakihubiri chuki bali upendo, amani na maendeleo kwa wananchi.
"Tumeuona mkono wa Mungu kwa kumrudisha kwetu Mheshimiwa Lissu, tutapita kwenye makanisa na misikiti kutoa shukrani kwa Mungu," amesema Heche wakati wa mkutano wa uchangiaji uliofanyika makao makuu ya Chadema wilayani Tarime. Sh3,134,500 zimekusanywa.
Mwenyekiti wa Chadema wilayani Tarime, Lucas Ngoto amesema, "Ni ukweli usiopingika kuwa Lissu hakuponywa na wanadamu, risasi alizopigwa ni nyingi lakini Mungu amekubali aendelee kuishi nasi hadi leo," amesema.
Peter Magwi ambaye ni katibu wa Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko amewataka wanachama na wapenda amani na maendeleo waendelee kutoa michango kusaidia matibabu ya Lissu.
"Maandiko katika vitabu vitakatifu yanasema usiogope. Watanzania tusiogope, tushauri na tukosoe kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu, kizazi cha sasa na  kijacho," amesema Magwi.

Wafanyakazi 143 Wa Ofisi Ya Rais Utumishi Wahamia Dodoma Awamu Ya Pili


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi. Dorothy Aidan Mwaluko akiagana na Kiongozi wa msafara wa magari yaliyobeba mizigo ya ofisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78. Katikati mwenye miwani Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bibi. Jane Kajiru.
Gari lililobeba nyaraka na vifaa vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora likijiandaa kuondoka katika viwanja vya ofisi hiyo iliyopo Magogoni leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwapungia mikono ya kwaheri madereva wa magari yaliyobeba mizigo ya ofisi hiyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kuhamia Dodoma leo Jijini Dar es Salaam. Jumla ya wafanyakazi 143 wameagwa katika awamu hii ya pili, ambapo awamu ya kwanza waliondoka wafanyakazi 78.

Aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na Historia yake


NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM


HISTORIA YAKE:

Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida.

Nyalandu alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani Singida na kuhitimu mwaka 1987. Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 – 1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.

Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari, Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (Ukwata) 1991 – 1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro, Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.

Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg.

Kabla ya hapo alikuwa amepata Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo. Kiongozi huyu, sasa ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diplomasia.

Baada ya kuhitimu masomo yake ughaibuni, Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West, akifanya kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.

Aliporejea nchini Tanzania alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).

Ushauri wa timu yake ulisaidia taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya, Marekani, China na nyinginezo. Pia, alikuwa anamsaidia mama huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya kitaifa na kimataifa.

Nyalandu amemwoa mrembo wa Tanzania mwaka 2004 ‘Miss Tanzania’, Faraja Kotta na wana watoto wawili, Sarah na Christopher.

MBIO ZA UBUNGE:

Tangu alipokuwa kijana mdogo, Nyalandu alionyesha kila dalili kuwa na nyota ya uongozi. Watu wanaomfahamu hawakushangaa walipomwona mwaka 2000 anaingia kwenye mpambano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akilisaka jimbo la Singida Kaskazini. Kutokana na udhaifu wa upinzani uliokuwepo wakati huo alijua atakuwa na kazi kubwa ndani ya chama chake tu, hivyo, alipopitishwa na CCM akapambana majukwaani na wapinzani na kuwa mbunge.

Mwaka 2005, Nyalandu alipitishwa tena na chama chake kuwania ubunge Singida Kaskazini, akakutana tena na upinzani dhaifu kutoka kwa Kimia Omari Rashid wa Chadema, akajivunia asilimia 93.5 ya kura zote na kuwa mbunge hadi mwaka 2010.

Baada ya kupata uzoefu wa ubunge, kwa miaka kumi, Nyalandu alirudi tena kutetea mara ya tatu; CCM ikampa nafasi mwaka 2010 na wananchi wakamchagua kwa ushindi wa asilimia 87.7 akimshinda kwa mara nyingine mgombea yuleyule wa Chadema wa mwaka 2005.

Ushindi wa mara hii ulikuja na bahati kubwa kwa Nyalandu. Bahati ya kwanza ilikuwa kukwea ngazi zaidi. Rais Jakaya Kikwete alimteua Nyalandu kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Novemba 2010 na alidumu hapo hadi Mei 2011 alipohamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, nafasi aliyokaa kwa takriban miaka mitatu.

Bahati ya pili, Januari 2014, nyota yake ilipaa zaidi akapewa wadhifa mkubwa; mara hii akiteuliwa kuwa waziri kamili wa Maliasili na Utalii, sekta ambayo ina changamoto kubwa sana hapa nchini na sekta hiyo nyeti ambayo imenufaisha mamia ya nchi duniani huku Tanzania watu wengi wakisema utalii haujalisaidia taifa kwa kiasi kinachofaa.

MBIO ZA URAIS:

Nyalandu aliweka wazi nia yake ya kuwania urais Desemba 28, 2014 na alitangaza nia hiyo ya kugombea urais katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Ilongero, katika jimbo analoliongoza, Singida Kaskazini, wakati akihutubia mamia ya wananchi.

Katika mkutano huo alisisitiza kuwa “sasa ni zamu ya vijana kuongoza nchi” huku akiwaambia wananchi kuwa safari yake ya ubunge kwa miaka 15 inaanzisha safari nyingine bila kuwaeleza ikiwa bado ana nia na ubunge au la. Aliambatana na mkewe, watoto wake pamoja na wazazi wake.

Kabla ya kutangaza nia ya urais, Nyalandu aliwahi kusikika akisema kuwa “…siwezi kutangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao bila kutumwa na watu” lakini kabla watu wenyewe hawajamtuma aliibuka na kuwaita yeye mwenyewe mkutanoni na kuweka nia yake.

Kwa nini marafiki zangu wa kike hutumiana picha za utupu

Kwa nini marafiki zangu wa kike hutumiana picha za utupuHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionKwa nini marafiki zangu wa kike hutumiana picha za utupu
Simu ya Gita's inalia. Anaichukua na mara kwa ghafla picha inajitokeza katika skrini .
Picha ya selfi kutoka kwa rafikiye mkuu akiwa utupu inajitokeza.
Gita anacheka na kutuma emoji tano za ishara ya moto na ujumbe "On fire girl." akimsifu.
Hakuna uhusiano wowote wa kingono kati ya Gita na rafikiye mkubwa.
Lakini mara kadhaa kwa wiki wanatumiana picha za utupu.
''Nilianza wakati nilipokuwa bila mpenzi'', anasema Gita mwenye umri wa miaka 26.
Nilikuwa nikihisi nimewachwa nje ya watu wanaotumiana ujumbe wa picha za utupu kwa sababu sikuwa na mtu wa kumtumia picha za utupu.
Ni njia ya kuwaonyesha marafiki zangu nilivyo na mwili mzuri.
Na hivi karibuni nimeanza kuweka mzaha. Ninaweza kutuma picha moja ya selfi ikiwa na titi langu likiwa wazi. Inatufanya tunacheka.
Yeye na marafikize sio wao pekee wanaotumiana picha za utupu .
Kile ambacho kilikuwa njia ya kuwachochea wapenzi kushiriki katika tendo la ngono sasa kinatumiwa kama ishara ya umoja na kuwezeshana miongoni mwa wanawake.
Selfi za utupu ni njia mojawapo ya kupigania imani ya kibinafsi , alielezea mmoja wa marafiki zangu Daisy Walker mwenye umri wa miaka 27 ambaye alikuwa mpiga picha wa fesheni wa zamani .
Daisy Walker
Image captionDaisy Walker
Imenichukua muda mrefu kukiuka mipaka ya urembo wa mwanamke na kuukubali mwili wangu.
Sasa, nina fursa ya kutojali iwapo watu wananitazama kuwa mrembo ama la.Hujiangalia mwili wangu nikiwa uchi na kufikiri, 'Kweli''.
Mimi ndiye hupokea picha zake za utupu , ambazo huzituma baada ya kuoga ama wakati anapopiga mswaki na huwa siogopi kuzitazama.
Sababu za Daisy kufanya hivyo zinafurahisha.
''Nadhani kwa mwanamke kukuwa katika jamii na kuchukua hatua ya kuukubali mwili wake ni mafanikio na nataka kuwasambazia hilo rafiki zangu'', alisema.
Natumai itasambaa kama moto wa msituni.
Alianzisha kundi la WhatsApp hususan kwa marafikize kusambaziana picha za utupu.
Daisy alianzisha kundi la WhatsApp hususan kwa marafikize kusambaziana picha za utupu.Haki miliki ya pichaINSTAGRAM
Image captionDaisy alianzisha kundi la WhatsApp hususan kwa marafikize kusambaziana picha za utupu.
Mmoja wa wanachama anasema kuwa nina picha nyingi za marafiki wangu katika simu.
Ni hatua yenye lengo la kusambaziana picha za urembo wetu kati yetu
Hatahivyo kutumiana picha za utupu ni hatari, unaweza kuwa rafiki na mtu unayemtumia picha lakini punde urafiki huo unapokatika picha hizo zinaweza kuwafikia watu wengine kwa lengo la kulipiza kisasi.

Ninja mwizi mwenye umri wa miaka 74 akamatwa Japan

Ninja wa Hisei aliyekamatwa kwa tuhuma za wizi JapanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNinja wa Hisei aliyekamatwa kwa tuhuma za wizi Japan
Maafisa wa polisi wa Japan wanasema kuwa hatimaye wamemkamata mwizi mmoja ambaye alikuwa amevaa vazi la ninja na walishangaa walipogundua kwamba ana umri wa miaka 74.
Baada ya kujifunika uso alinaswa na kamera ya usalama mwaka huu, na aliwekwa chini ya uchunguzi na kupelekea kukamatwa kwake mnamo mwezi Julai.
Maafisa wa polisi wanaamini ndiye ninja kwa jina ''Ninja wa Heisei'' anayedaiwa kuvunja na kuiba katika maeneo 250.
Ameshtakiwa na wizi wa thamani ya Yen milioni 30 za Japan {$260,000}.
Polisi walikuwa wameshangazwa na misururu ya wizi wa kuvunja kwa kipindi cha miaka minane uliofanywa na mshukiwa aliyekuwa akivalia nguo nyeusi wakidhania kwamba umefanywa na mtu aliye na umri mdogo.
Wachunguzi walimchunguza mshukiwa huyo ambaye wanasema alionekana kuwa tofauti na watu wengi wa umri mkubwa.
Lakini wanasema kuwa baadaye alienda katika jengo moja lisilo na watu na kubadilisha nguo zake na kusubiri hadi usiku ulipoingia ili kuiba.
''Alikuwa amevalia vazi jeusi linalomfunika mwili mzima isipokuwa macho'' , alisema faisa mmoja mwandamizi magharibi mwa mjini wa Osaka nchini Japan.

Polisi watumia pesa kama chakula na mswaki Afrika Kusini

Noti
Polisi wawili wa trafiki nchini Afrika Kusini wamesimamishwa kazi na wanakabiliwa na mashtaka ya kuaibisha kikosi cha polisi baada ya video yao "wakila pesa" kusambaa sana mitandao ya kijamii.
Video hiyo inawaonesha polisi hao wawili wakitumia noti za pesa kuchonokoa meno yao na pia kujipangusa, huku muziki wa sauti ya juu ukisikika kwenye gari lao.
Wawili hao wanaonekana pia wakila chakula chao cha mchana kutoka kwenye mikebe ya Styrofoam kwenye sehemu ya kubebea mizigo nyuma ya gari.
Mikebe hiyo nusu imejazwa pesa na nusu pesa.
Idara ya polisi wa jiji la Ekurhuleni amesema wafanyakazi hao, ambao wamevalia sare rasmi ya polisi wakati huo, wameiaibisha idara hiyo na kwamba vitendo hivyo si vya kistaarabu.
Msemaji wa idara hiyo Wilfred Kgasago amesema wawili hao wamekabidhiwa barua za kuwasimamisha kazi mapema na kwamba watafika katika kamati ya nidhamu Jumanne.
Waziri wa polisi nchini Afrika Kusini Fikile Mbalula alipakia video hiyo kwenye Twitter mwishoni mwa wiki, na akafurahia hali kwamba wawili hao wataadhibiwa.

Kiongozi wa upinzani Tanzania Zitto Kabwe aachiwa na kukamatwa tena

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe
Image captionMbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe
Zitto Kabwe , kiongozi mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT Wazalendo, aachiwa na kukamatwa tena kwa maelekezo ya ofisi ya afisa upelelezi imakosa ya jinai.
Mbunge huyo wa Kigoma mjini, alikamatwa mara ya kwanza asubuhi ya Jumanne nyumbani kwake mjini Dar es salaam na kupelekwa kituo cha polisi Chang'ombe.
Baada ya masaa kadhaa mbunge huyo aliachiliwa huru kabla ya kukamatwa tena.
Akizungumza na BBC, wakili wa Bwana Kabwe, Stephan Ally Mwakibolwa anasema sababu zilizotajwa kwa kushikwa kwake ni kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi.
"Kauli kubwa haswa wanayosema ni kuihusisha serikali ya CCM na matukio ya watu waliookotwa katika fukwe za bahari ya hindi wakiwa wamefariki ,pamoja na tukio la mbunge Tundu Lissu"
Bwana Kabwe sasa amepelekwa katika kituo cha polisi cha Kamata mjini Dar es salaam.

SWEDEN YATOA BILIONI 80/- KUCHANGIA MAENDELEO TANZANIA


UBALOZI wa Sweden nchini, umewekeana saini makubaliano na Umoja wa Mataifa na utatoa Sh bilioni 80.4 kwa shughuli za maendeleo ndani ya miaka minne.
Baada ya kutiliana saini, Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt, alisema wamechagua kusaidia shughuli za Umoja wa Mataifa zinazoakisi malengo ya maendeleo ya nchi katika nyanja za haki za wanawake, utawala wa demokrasia na ukuaji wa uchumi.
Alisema shughuli hizo ni zile ambazo  zinamnufaisha kila mmoja katika kipindi ambacho Tanzania inalenga kuwa na uchumi wa kipato cha kati.
“Kwa kupitisha sehemu ya msaada wetu kupitia Mfuko wa Umoja wa Mataifa chini ya mpango wa kufanya kazi pamoja, tunashiriki kikamilifu katika kusaidia ufikiwaji wa malengo ya maendeleo nchini Tanzania.
“Vile vile tunatambua bayana kabisa na kuthamini wajibu waliokubaliwa kuwa ndio wa Umoja wa Mataifa katika kuleta maendeleo endelevu,’’ alisema  Rangnitt.
Aliongeza kuwa kwa msaada huo wanawezesha uchukuaji unaoendana na sera ya nje inayozingatia haki za wanawake wa Sweden na pia jitihada  zinazolenga  ajira yenye hadhi na haki za watoto.
Aidha alisema wapo tayari kuendelea kuisaidia Tanzania na Umoja wa Mataifa pamoja na kuyapokea mageuzi ya mfumo wa UN chini ya mpango wa kufanya kazi pamoja na kutambua njia fungamanifu zinazotumika na thamani inayopatikana kutokana na mchango wa mashirika ya UN katika kushirikiana na Tanzania.
Mratibu  Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP , Alvaro  Rodriguez, alishukuru msaada huo endelevu  na kuipongeza Sweden kwa kuwa mshirika wa maendeleo asiyeyumba katika shughuli za UN na Tanzania.

MITA 60 BONDE LA MTO RUFIJI ZATESA WANANCHI


WATAALAMU wa Bonde la Mto Rufiji wamelalamikiwa kwa kushindwa kutoa elimu kwa wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe ili kufahamu sheria inayokataza watu  wasifanye shughuli za kibinadamu mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji.
Akizungumza wakati wa operesheni ya kuondoa mabomba ya maji yaliyowekwa na wananchi wanaofanya kilimo cha umwagiliaji pembezoni mwa bonde hilo, Diwani wa Kata ya Imalinyi, Onesmo Lyandala, alisema kama wananchi wake wangeelimishwa sheria za mita 60 wasingefanya kilimo hicho.
Operesheni hiyo ilitekelezwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Wanging’ombe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Ali Kassinge na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wanging’ombe (WANGIWASA).
“Mpaka sasa operesheni hii imekata miti, mabomba ambayo yalikuwa yakitumika katika kumwagilia, tumeichukua na itakua ni mali ya kijiji.
“Hata hivyo, hakuna mwananchi anaifahamu sheria ya mita 60 zinaanzia wapi na kuishia wapi, ”alisema Lyandala.
Mtaalamu wa Maji Bonde la Mto Rufiji, Abisai Chilunda, alisema hatua ya kuharibu miundombinu ya mabomba kwenye vyanzo vya maji katika bonde hilo, imetokana na usimamizi wa sheria namba 11 ya mwaka 2016 kuhusu rasilimali za maji.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AZITAKA TAASISI ZA FEDHA KUPUNGUZA RIBA YA MIKOPO

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizundua rasmi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania –TPB Bw. Sabasaba Moshingi baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimpongeza Mwenyekiti wa Kikundi cha Akiba na Mikopo-(KIKOBA) cha Mwende, Manispaa ya Dodoma, Bi. Bertha Chisawilo, baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, kumkabidhi Mwenyekiti huyo, Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na masuala ya fedha (Financial Sector Deepening Trust-FSDT), Bw. Sosthenes Kewe, baada ya Sera na Mkakati huo kuzinduliwa rasmi, mjini Dodoma.



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb), akichangia mada kuhusu umuhimu wa huduma za fedha hususan vijijini, kabla Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, hajazindua rasmi 




Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (Sera), akizungumza maneno ya utangulizi wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028,  iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.




Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akizungumzia mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali kwa kuja na Sera ya kuhudumia Sekta Ndogo ya Fedha nchini ijulikanayo kama Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028,  iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo (Mb), akielezea utayari wa Wizara yake katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea umuhimu wa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028 katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini katika jamii, wakati wa uzinduzi wa sera hiyo mjini Dodoma.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano serikalini-Wizara ya Fedha nan Mipango



Na Benny Mwaipaja, Dodoma


MAKAMU wa Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN, amezinduzi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, tukio  litakalofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoa huduma ndogo za fedha kupunguza riba za mikopo na tozo mbalimbali ili kufanikisha lengo la Sera hiyo ambalo ni kuimarisha huduma jumuishi za fedha kwa kujenga mazingira wezeshi yatakayoleta ufanisi wa utoaji wa huduma ndogo za fedha nchini kwa wananchi wenye kipato cha chini.

“Ninawaomba pia muongeze ubunifu katika kutoa huduma zinazohitajika na wananchi wa kipato cha chini pamoja na kupeleka huduma hizo katika maeneo yaliyo karibu na makazi yao au biashara zao” aliongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan

Alizitaka taasisi za huduma za fedha kuwaelimisha wananchi kabla ya kutoa huduma hizo ili kupunguza athari wanazozipata wananchi.

“Ni matarajio yangu kuwa, Wizara ya Fedha na Mipango itashirikiana na wadau katika kutekeleza Sera hii na kuhakikisha malengo ya Sera ambayo ni   kukuza uchumi na kupunguza umaskini yanafikiwa” alisisitiza

Alisema Ripoti ya Finscope ya mwaka 2017 ambayo iilionesha kuwa Tanzania imepiga hatua kwenye suala zima la huduma jumuishi za fedha (financial inclusion) na kufikia asilimia 72 kwa 2017, huku changamoto kuu iliyoainisha ni elimu/uelewa mdogo wa huduma za fedha kwa wananchi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alisema kuwa Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake itaweka mazingira yatakayowezesha kuchochea maendeleo stahiki na ubunifu wa Huduma Ndogo za Fedha ili kukidhi mahitaji halisi ya wananchi wa kipato cha chini na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Alisema kuwa Sera hiyo itaongeza utoaji wa huduma bora na jumuishi ya Kifedha Vijijini na kutungwa kwa sheria ambazo zitawalinda wananchi dhidi ya baadhi ya taasisi za kifedha zinazoibuka na kuwa kero kwao kwa kuweka riba kubwa pamoja na kupatiwa huduma zisizoridhisha.

“Sera ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake vitaendelea kutoa miongozo kwa wadau wote na kuchochea uanzishwaji wa washiriki wapya na ukuaji wa waliopo ili kutoa ushindani zaidi ili kuleta matokeo yatakayoongeza huduma rasmi, kukuza utamaduni wa kuweka akiba, kuimarisha sekta ndogo ya fedha, ambayo yatachangia ukuaji wa uchumi, ajira na kupunguza umaskini” Aliongeza Dkt. Mpango

Sekta ya huduma ndogo ya fedha nchini inajumuisha aina ya watoa huduma za fedha wafuatao: benki na taasisi za fedha zinazotoa huduma ndogo za fedha; vyama vya ushirika wa kuweka akiba na kukopa; kampuni za huduma  ndogo za fedha kama vile BRAC, Blue Finance, Tujijenge, Platinum n.k,

Nyingine ni asasi za fedha zisizo za Serikali, Mifuko na Programu za Serikali; na Vikundi vya Kifedha vya Kijamii kama vile asasi za kijamii, benki za kijamii za vijiji (VICOBA), Ushirik a wa akiba na mikopo vijijini (VSLAs), Ushirika wa akiba na mikopo kwa zamu (ROSCAs), wakopeshaji binafsi na wengine wanaotoa huduma zinazohusiana na fedha.

Serikali kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa Huduma Ndogo za Fedha kwa wananchi wa kipato cha chini iliamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2000 kwa kutunga Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wa Sera hiyo kwa kipindi cha miaka kumi ili kutatua changamoto zilizojitokeza katika sekta ndogo ya fedha

Changamoto hizo ni pamoja na ongezeko la idadi ya watoa Huduma Ndogo za Fedha; Ukosefu wa mfumo wa Sheria na Kanuni za kusimamia Taasisi Zisizochukua Amana na Vikundi vya Fedha vya Kijamii; Ukosefu wa mfumo wa kumlinda Mtumiaji na mtoa Huduma Ndogo za Fedha na uelewa mdogo wa masuala ya fedha; Kutokuwepo na uwazi katika vigezo na masharti ya utoaji mikopo; Viwango vya juu vya riba; na Kuibuka kwa taasisi zisizo kuwa na uaminifu.