Maafisa wa polisi wa Japan wanasema kuwa hatimaye wamemkamata mwizi mmoja ambaye alikuwa amevaa vazi la ninja na walishangaa walipogundua kwamba ana umri wa miaka 74.
Baada ya kujifunika uso alinaswa na kamera ya usalama mwaka huu, na aliwekwa chini ya uchunguzi na kupelekea kukamatwa kwake mnamo mwezi Julai.
Maafisa wa polisi wanaamini ndiye ninja kwa jina ''Ninja wa Heisei'' anayedaiwa kuvunja na kuiba katika maeneo 250.
Ameshtakiwa na wizi wa thamani ya Yen milioni 30 za Japan {$260,000}.
Polisi walikuwa wameshangazwa na misururu ya wizi wa kuvunja kwa kipindi cha miaka minane uliofanywa na mshukiwa aliyekuwa akivalia nguo nyeusi wakidhania kwamba umefanywa na mtu aliye na umri mdogo.
Wachunguzi walimchunguza mshukiwa huyo ambaye wanasema alionekana kuwa tofauti na watu wengi wa umri mkubwa.
Lakini wanasema kuwa baadaye alienda katika jengo moja lisilo na watu na kubadilisha nguo zake na kusubiri hadi usiku ulipoingia ili kuiba.
''Alikuwa amevalia vazi jeusi linalomfunika mwili mzima isipokuwa macho'' , alisema faisa mmoja mwandamizi magharibi mwa mjini wa Osaka nchini Japan.
No comments:
Post a Comment