Nairobi, Kenya. Kenya imekuwa ikisubiri kwa shauku kubwa siku ya Jumanne ambayo kiongozi wa upinzani Raila Odinga amejiandaa kutoa hotuba juu ya mikakati waliyonayo baada ya kususia uchaguzi wa marudio uliomwezesha Rais Uhuru Kenyetta kupata ushindi wa kishindo.
Kenyatta alitangazwa jana kuwa mshindi wa uchaguzi huo wa Alhamisi kwa asilimia 98 ya kura zilizopigwa matokeo yanayothibitisha hata uchaguzi wa awali wa Agosti 8 alikuwa ameshinda japo yalibatilishwa na Mahakama ya Juu.
Hata hivyo ushindi wa Kenyatta una utamu wenye uchungu. Idadi ya asilimia 38.8 ya watu waliojitokeza inatarajiwa kuibua maswali juu ya kuaminika kwa uchaguzi huo ulioigawa nchi katika pande mbili na kuchochea mapambano ya kisheria na maandamano ya ghasia yaliyodumua miezi kadhaa.
"Kilichofanyika hapa si kingine bali kuhalalisha matakwa ya wapigakura,” alisema Kenyatta katika hotuba yake ya kupokea ushindi huku akikiri uwezekano wa matokeo hayo kukumbwa na changamoto za kisheria.
Upigaji kura wa Alhamisi ulijaa matatizo kama vituo kuzuiwa kutokana na vurugu kwenye kaunti nne za Nyanza zilizofanywa na wafuasi wa Odinga waliosusia na kusababisha siku mbili za mapambano na vikosi vya usalama. Watu tisa waliuawa.
Hadi jana, Odinga alikuwa kimya lakini amewaahidi wafuasi wake atatoa tam
No comments:
Post a Comment