Wednesday, November 15

Dk Shika atimiza ahadi ya polisi


Dar es Salaam. 'Bilionea' Dk Louis Shika aliyeibuka mshindi wa kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi leo Novemba 15  ameripoti kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam kama alivyotakiwa.
Dk Shika ameripoti kama alivyotakiwa jana na Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa mara baada ya kuachiwa kwa kujidhamini yeye mwenyewe.
Kabla ya kwenda kuripoti, Dk Shika ambaye amekuwa maarufu kila anapopita, alipata kifungua kinywa maeneo ya Posta.
Saa 2.24 asubuhi, Dk Shika alikuwa amewasili kituoni hapo na ilipofika Saa 3.36 asubuhi aliondoka na kesho atarejea tena kituoni hapo.
Akizungumza na Mwananchi lililokuwapo tangu anaingia hadi anatoka amesema hana tatizo na ataendelea kuitikia wito wa polisi bila tatizo.

No comments:

Post a Comment