Walimu hao walijikuta wamelala nje kimazingira katika Kisiwa cha Soswa
Buchosa. Wananchi wa Kisiwa cha Soswa halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamewatupia mpira walimu waliojikuta wamelala nje kwa madai ya imani za kishirikina kuwa ni tukio la kutengenezwa.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa jana Alhamisi kwa dharura kujadili suala hilo lililojitokeza usiku wa kuamkia Novemba 15, mwaka huu, katika viwanja vya shule ya msingi Soswa wananchi hao walisema tukio hilo ni la kutengenzwa ili kuishinikiza Serikali iwape uhamisho kutokana na mazingira magumu wanayokaa.
Mzee wa kisiwa hicho, Mashinga Boniphace (80) alisema hakuna ukweli juu ya tukio hilo kwani yeye pamoja na wazee wenzake waliangalia vibuyu na damu iliyokuwa imetapakaa ndani ya nyumba za walimu hao sio ya kishirikina.
“Walimu hao waliamua kuua ndege aina ya nyagenyange ili na kutapakaza damu hizo ndani ya nyumba zao pamoja na kwenye vibuyu ili kushinikiza uongozi wa juu kuwahamisha kutokana na juhudi zao za kuhama kugonga mwamba,”alisema Boniphance
Kauli ya mzee huyo wa mila ilipingwa na mkazi mwingine wa kijiji hicho, Mjula Magafu ambaye alisema suala hilo liangaliwe kwa kina kwakuwa limezua sintofahamu ndani ya kisiwa hicho na Taifa kwa ujumla.
Alisema kama walimu ndio walitengeneza tukio hilo wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa kudanganya umma.
“Hapo awali lilipotokea tukio la nyumba zao kupondwa mawe walimu wote waliondoka na kubaki wawili ambapo hakukuwa na kitendo kama hicho, baadaye walimu waliokuwa wamesusia akiwemo mwalimu Daudi Shule na Wape Kisimu kitendo hicho kilijirudia tena na sasa wameamua kutengeneza tukio la kulazwa nje, tunapaswa kuchunguza kwa kina,” alisema Magafu
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na Mwananchi walisema tukio hilo limewaathiri kimasomo hivyo kushindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Mwanafunzi wa darasa la tano, Malisela James aliiomba jamii ikubali kuwa walimu hao wamefanyiwa vitendo vya kishirikina na kwamba watafute namna ya kukukomesha ili kuwapa fursa ya kuendelea kusoma.
Mwenyekiti wa kamati ya shule, Lidia Buluba alilaani kitendo hicho ambacho kinahisishwa na imani za kishirikina huku akiwatupia lawama baadhi ya walimu waliotengeneza jambo hilo ili wapatiwe uhamisho kwa madai kuwa mazingira wanayoishi si mazuri.
Mwalimu Daudi Shule ambaye anapatiwa matibabu ya asili katika kijiji cha mwangakia yeye alidai alinyolewa sehemu za siri, mwalimu Ernest Katunzi alithibisha kwa kumwona sehemu hizo kuwa amenyolewa pamoja na mwalimu Wape Kisumo aliyonyolewa nywele kichwani kwa pamoja walisema kuwa wanafanyiwa vitendo vya kishirikina hata kipindi wanapondwa mawe jamii hiyo haikuamini.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Petro Lukas alisema maneno yanayosemwa na jamii hawawezi kuyaamini na haamini kama walimu wametengeneza mazingira ya tukio hilo ili wahame kwa kuwa kazi yao ni kufundisha.
Mtendaji wa Kata ya Bulyaheke, Musa Mwilomba alisema kuwa anaiomba jamii kutokutupiana mpira juu ya tukio hilo na kwamba wanatakiwa kusameheana na kusahau kilichotokea ili kuanza sura mpya na walimu waendelee kufundisha.
Mkaguzi wa shule wilayani Sengerema, Elly Msulu aliyefika katika Kisiwa cha Soswa kupata ukweli juu ya tukio hilo aliitaka uchunguzi zaidi ufanyike kujua ukweli wa tukio hilo na watakaobainika hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa huku akiwaomba walimu kuwa wavumilivu wakati suala hilo linatafutiwa ufumbuzi.
Unaweza ukawa ndio mwisho wa zama za utawala wa Rais Robert Mugabe, ambaye ameitawala Zimbabwe tangu mwaka 1980.
Mpaka jana jioni, Mugabe alikuwa kizuizini nyumbani kwake baada ya jeshi la nchi hiyo kuingia mitaani, huku likidai kuwa na dhamira ya kuwashughulikia linalowaita wahalifu wanaomzunguka rais huyo.
Kimsingi, hatua ya jeshi hilo inaonekana kuleta mjadala mkubwa kutoka kwa watu wengi ndani na hata nje ya bara la Afrika.
Kuna wanaounga mkono utawala wa Mugabe na kuna ambao wanapinga kwa madai kuwa ametawala muda mrefu.
Si Mugabe pekee, duniani kuna viongozi kadhaa ambao wamekaa madarakani kwa muda mrefu ama kwa sababu katiba zao hazijaweka ukomo au zimebadilishwa mara kwa mara kwa lengo la kuwabeba.
Kwa viongozi ving’ang’anizi kama Mugabe, kibaya zaidi kwao si tu kujimilikisha uongozi wa nchi, lakini wanaporuhusu watu wao wa karibu hususan wanafamilia kufanya wayatakayo. Wanafamilia hawa hawaguswi na vyombo vya dola, hakuna anayewanyooshea kidole hata kama wanayofanya yanazipeleka nchi zao shimoni. Ikumbuke kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho; viongozi wajifunze kukubali kuwapo kwa ukomo wa madaraka. Hakuna mwenye hakimiliki ya kuongoza nchi hata kama atakuwa ameifanyia makubwa nchi yake.
Tujifunze kutoka kwa Mwalimu Julius Nyerere, ambaye kwa mchango aliotoa katika uhuru wa Tanzania, pengine mpaka sasa nchi hii ingeweza kuwa chini ya utawala wa kizazi chake. Harakati za kufa na kupona alizofanya na waasisi wenzake yeye akiwa kama kinara hazikumpa jeuri za kuona ana haki ya kutawala nchi milele; ndio maana aliamua kung’atuka na kuwapisha wengine kuongoza nchi.
Mwalimu Nyerere hakung’atuka kwa sababu alichokwa, ila alisukumwa na busara ya kuona kuwa kulikuwa na haja ya kumpisha mwingine kuongoza nchi. Kitendo cha aina hii pia kilifanywa na Nelson Mandela aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini.
Mugabe (93) licha ya kuongoza kwa muda mrefu wa miaka 37, alitaka kumuachia madaraka mkewe Grace jambo ambalo linaonekana kupingwa na watu wengi wakiwemo wanajeshi hao ambao wamemuweka kizuizini. Wanaompinga wanasema Zimbabwe ilihitaji mtu mpya mwenye maono mapya.
Kadhia ya Zimbabwe haina budi kuwa tanbihi kwa viongozi wengine barani Afrika; bara ambalo mpaka tunaandika maoni haya limegubikwa na viongozi wengi wabinafsi na wapenda madaraka.
Rai yetu kwa viongozi wa Afrika na dunia kwa ujumla, wakubali kuwapo kwa mfumo wa kubadilishana madaraka. Na hii ndiyo demokrasia kama anavyosema Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu) kuwa ni lazima serikali za Afrika ziweke sawa mazingira ya ushindani wa kisiasa katika kuongoza nchi.
Bara la Afrika linahitaji maendeleo stahimilivu ili kuwakomboa wananchi wake katika lindi la changamoto za kimaisha ukiwamo umasikini uliovuka ada. Ili tufike huko nchi zetu hazina budi kuheshimu na kutekeleza misingi ya demokrasia, utawala bora na utii wa sheria.
Hakuna popote anayeweza kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi, lakini ni busara kwa viongozi wanaotawala kuwa na busara na kufuata misingi ya Katiba ili kuepusha mambo kama hayo.
Muleba. Polisi wanamshikiliwa mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Kagoma wilayani Muleba, kwa kosa la kuwaua pacha wake.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Augustino Olomi alisema tukio hilo lilitokea Novemba 14 baada ya mwanamke huyo kuwanyonga watoto wake na kusingizia kuwa wamefariki dunia. “Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha mauaji ya watoto hao, itakapojulikana hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” alisema Olomi.
Naye mwenyekiti msaidizi wa kijiji hicho, Patrick Luhosho alieleza mwanamke huyo aliwaua watoto wake hao wenye mwezi mmoja na kuzika miili yao Kitongoji cha Nundu kilichopo katikati ya kijiji jirani cha Buhaya.
Luhosho alisema taarifa za tukio hilo zilipatikana baada ya ndugu kuanza kuhoji walipowekwa watoto hao na kwamba, aliwaeleza kuwa wamefariki.
“Taarifa hizo ziliwashtua wananchi kwani hivi karibuni alikuwa akidai anakosa huduma ya kuwatunza pacha hao kutokana na ugumu wa maisha,” alisema.
Alisema baada ya polisi kuwasili kijijini hapo kufanya uchunguzi, aliwaeleza kuwa watoto walifariki na kuzikwa Kijiji cha Nshamba lakini walipofuatilia walibaini ni uongo. “Wananchi wanaendelea kutafuta miili hiyo kwa kutumia mbwa,” alisema Luhosho.
Mwanamke huyo ambaye ni uzazi wake wa tano, anadaiwa kuwaua watoto wake hao ambao amezaa na mwanaume ambaye hajafahamiki baada ya kuachika kwenye ndoa yake ambako alizaa watoto wanne.
Ameshinda tuzo hizo katika masuala ya nishati na miundombinu
Addis Ababa-Ethiopia. Mwandishi mwandamizi wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Nuzulack Dausen ameshinda tuzo ya mwandishi bora Afrika wa masuala ya nishati na miundombinu katika tuzo za umahiri wa habari Afrika za Zimeo zilizotolewa jana Alhamisi usiku jijini hapa.
Zimeo ambazo zimetolewa kwa mara ya tatu sasa ni tuzo maarufu katika tasnia ya habari barani Afrika sambamba na tuzo za CNNMultichoice ambazo zimekuwa zikitolewa kila mwaka.
Tuzo hizo za Zimeo hutolewa na shirika linaloshughulikia ukuaji wa tasnia ya habari Afrika ya African Media Initiative (AMI) yenye makazi yake jijini Nairobi, Kenya na kudhaminiwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa yakiwemo Unesco, Kamisheni ya Uchumi ya Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) na Shirika la Habari la Al-Jazeera.
Katika kipengele cha nishati na mazingira, Dausen alikuwa akichuana na wanahabari Jeffrey Moyo ambaye huandikia Shirika la Habari la Thomson Reuters na The New York Times na Femi Asu wa gazeti la The Punch la nchini Nigeria.
"Kwanza namshukuru Mungu kwa tuzo hii ya heshima katika maisha yangu ya uandishi wa habari na nawashukuru viongozi na wafanyakazi wenzangu wa MCL kwa kunijenga kitaaluma na kunitia moyo kwa kila nachojaribu kukifanya.
"Pia nawashukuru familia yangu kwa kunipa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kukubali kunikosa kwa muda napokuwa katika majukumu ya kazi nje ya Dar es Salaam na wasomaji ambao maoni yao hunijenga zaidi," amesema Dausen.
Dausen, ambaye ni mhariri wa habari za takwimu wa MCL, amesema uhuru wa habari na uandishi mahiri wa habari unaochambua masuala kwa kina utasaidia kuchochea maendeleo Tanzania na duniani kwa ujumla kwa kuainisha fursa na kutoa majibu ya changamoto zinazoikabili jamii.
Habari iliyompa ushindi Dausen inahusu namna wakazi wa vijiji vya Namikango A na B wilayani Nachingwea mkoani Lindi Tanzania walivyotumia fursa ya umemejua kupata mwanga na kukabiliana na umaskini. Habari hiyo ilichapwa katika gazeti dada la The Citizen zaidi ya miezi miwili iliyopita.
Akizungumzia vigezo vya utoaji tuzo hizo, Jaji Mwandamizi katika tuzo hizo Dk George Nyabuga wa Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) amesema walizingatia vigezo vingi vya kihabari vikiwemo uhalisia wa wazo la habari, mpangilio wa hoja na umahiri wa kueleza habari hiyo ikaeleweka na wananchi wa kawaida. Vigezo vingine ni namna mada husika inavyowagusa wananchi, matumizi ya takwimu na uzingatiaji misingi ya habari ya usawa, weledi, na ukweli.
"Haikuwa kazi rahisi kuchambua mamia ya kazi za wanahabari Afrika nzima hadi kupata washindi wetu leo, " amesema Dk Nyabuka.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa AMI, Erick Chinje amesema ili vyombo vya habari viwe na msaada kwa watu wa Afrika ni lazima tasnia ya habari iboreshe utendaji wake kwa kuripoti na kuchambua masuala yanayogusa wananchi. "Mchango wa AMI umekuwa katika kuandaa mipango ambayo itawasaidia wanahabari kuongeza uwezo wao kitaaluma na mbinu nyingine zitakazofanya wawe bora zaidi. Tuzo za Zimeo zitawatambua wanahabari waliofanya vyema katika kuripoti sekta muhimu katika maisha ya watu," amesema Chinje.
Baadhi ya wanahabari walioshinda tuzo hizo jana usiku ni Dorcas Wangira kutoka Kenya, Ridwan Dini-Osman kutoka Ghana na Jay Caboz wa Afrika Kusini aliyeibuka mshindi wa jumla wa tuzo hizo
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMfumo wa treni Japan ni wa kutegemewa sana
Shirika moja la reli Japan limeomba radhi baada ya moja ya treni zake kuondoka sekunde 20 mapema.
Wasimamizi wa shirika la treni za reli ya Tsukuba Express kutoka Tokyo hadi Tsukuba wanasema wameomba radhi sana kwa usumbufu ambao huenda waliwasababishia wasafiri.
Kupitia taarifa, shirika hilo limesema treni hiyo ilikuwa imepangiwa kuondoka saa 9.44.40 (Saa tatu na dakika arobaini na nne na sekunde arobaini na nne) lakini iliondoka saa 9.44.20.
Wengi wa watu mitandaoni, hasa kutoka mataifa mengine wameshangazwa sana na hatua ya shirika hilo.
Shirika hilo limesema kosa hilo lilitokana na hatua ya wafanyakazi wake kutoangalia vyema ratiba ya treni kabla ya kuondoka.
Wameongeza kwamba hakuna mteja yeyote aliyelalamika kutokana na hatua ya treni hiyo kuondoka mapema kutoka kituo cha Minami Nagareyama kaskazini mwa Tokyo.
Tsukuba Express huwasafirisha abiria kutoka Akihabara mashariki mwa Tokyo hadi Tsukuba kwa dakika 45.
Ni nadra sana kwa treni Japan, nchi iliyo ya mfumo wa treni wa kuaminika sana duniani, kuondoka wakati ambao haipangiwi kuondoka.
Reli ya Tokkaido, inayotoka Tokyo hadi Kobe, husafirisha watu karibu 150 milioni kila mwaka.
Ndege iliyokuwa imembeba Raila ilitua wakati polisi wakipambana na wafuasi wake ambao walikuwa wakihaha kuingia ndani ya kiwanja hicho kilichokuwa chini ya ulinzi mkali hali iliyosababisha kupambana na polisi.
Nairobi, Kenya. Pamoja na ulinzi mkali uliowekwa kuzuia wafuasi wa Nasa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyetta (JKIA) baadhi wamemudu kufika ili kumpokea kiongozi wao Raila Odinga akitokea katika ziara ya siku 10 nje ya nchi.
Raila aliyekwenda Marekani kulalamikia jinsi ulivyofanyika uchaguzi mkuu wa marudio kwa kura ya urais nchini Kenya alitua JKIA saa 5:00 asubuhi.
Ndege iliyokuwa imembeba Raila ilitua wakati polisi wakipambana na wafuasi wake ambao walikuwa wakihaha kuingia ndani ya kiwanja hicho kilichokuwa chini ya ulinzi mkali hali iliyosababisha kupambana na polisi.
Licha ya ulinzi huo na moshi wa mabomu ya machozi wafuasi wa Nasa wapatao 200 wakiwemo wanawake walifanikiwa kupita utepe uliowekwa na vyombo vya usalama na wakaingia hadi ndani ya uwanja.
Helikopta ya polisi ilikuwa ikizunguka juu ya uwanja huo huku magari ya maji ya kuwasha na magari ya maalumu ya kusafisha njia yalikuwepo uwanjani hapo na yalitumika kuzima moto wa matairi.
Jana Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na mwenzake wa Rauaraka TJ Kajwang na mwanasiasa wa Starehe Steve Mbogo walikamatwa na polisi.
Heche amesema amepokea wito kuwa anatakiwa akahojiwe Morogoro
Dodoma. Polisi wanaoelezwa kutoka mkoani Morogoro wako eneo la Bunge ikielezwa kuwa wanakusudia kumkamata Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Heche, zimesema polisi hao wanamhitaji ili apelekwe Morogoro.
"Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.
Mbunge huyo amesema hajui kosa alilotenda, isipokuwa anatakiwa kuhojiwa kwa kauli alizotoa Machi mwaka huu alipomsindikiza Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali alipotoka gerezani.
Image captionBalozi wa Switzerland nchini Tanzania Florence Tinguely Mattli
Kampuni kutoka nchini Uswisi imefungua kiwanda cha kemikali za ujenzi na zile zinazotumika katika magari.
Florence Tinguely Mattli ni balozi wa Uswisi nchini Tanzania, ameiambia BBC kuwa suala la uwekezaji ni hatua ya kujiamini kwanza na kutoona hasara.
Alipoulizwa kuhusiana na sera za uwekezaji nchini Tanzania kudaiwa kuwa si rafiki Bi.Mattli amesisitiza kuwa uzoefu wao kiviwanda na kuwekeza katika mataifa mbalimbali duniani itawasaidia kujua ni mambo gani ya kuzingatiwa katika uwekezaji wao Tanzania katika serikali ya awamu ya sasa.
Image captionKiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu moja
Waziri wa viwanda wa Tanzania Dr Charles Mwijage anasema kuwa dira ya mwaka 2025 ni kuhusiana na viwanja.
Meneja mkuu wa kiwanda hiki cha Kemikali cha Sika Tanzania Alfonso Paradinas anasema kiwanda chake kitazalisha kemikali hizo za ujenzi na kuongeza ubora wa majengo nchini humo.
Hata hivyo kwa upande wake Meneja wa kanda ya Sika ya Ulaya, Mashariki ya kati na Afrika Ivo Schaedler lengo lao ni kutumia soko la Tanzania na kuongeza ufanisi nchini humo,na kuongeza kuwa wana viwanda 17 ndani ya Afrika.
Haki miliki ya pichaANAND BORA/SANCTUARY NATURE FOUNDATIONImage captionWanakijiji na walinzi walimuokoa chui huyo kwa kurusha ndani kitanda kwenye kisima
Mnamo Julai 19, 2012, Anand Bora alipokea simu isiyo ya kawaida saa mbili asubuhi na kufahamishwa kwamba chuo alikuwa amekwama kwenye kisima katika kijiji kimoja jimbo la Maharashtra, magharibi mwa India.
Bw Bora alikimbia kwenye kijiji hicho cha Bubali na kupiga picha operesheni ya zaidi ya saa tatu unusu ya walinzi wa msitu na wanakijiji wakijaribu kumuokoa chui asife maji kisimani.
Ni mwalimu lakini mpiga picha na alipiga picha za kipekee siku hiyo.
Katika moja ya picha hizo, chui huyo kuwa anaonekana akitazama juu kuwaangalia wale waliokuwa wanamuokoa.
Picha hizo ilishinda tuzo ya upigaji picha wa wanyamapori nchini India wiki iliyopita.
Ushindi wake umeibua maswali kuhusu yaliyojiri wakati wa uokoaji huo.
Picha hiyo ya miaka mitano iliyopita ni ya kipekee kwani mara nyingi wanyamapori hushambuliwa na kuuawa na wakazi.
"Chui huyo alipotazama juu, anaonekana kuhisi kwamba hatungemuumiza, kwamba tulikuwa tunajaribu kumuokoa," Bw Bora ameambia BBC.
Haki miliki ya pichaANAND BORAImage captionChui mara nyingi hudungwa sindano ya kuwatuliza au kunaswa kwa kutumia nyavu na baadaye kuachiliwa huru porini, mfano huyu aliyeokolewa Nashik Desemba 2010
Maafisa wa msitu walipofika, wanakijiji waliwafahamisha kwamba chui huyo alikuwa ameogelea kisimani kwa saa 25 akijaribu kujizatiti asizame.
Mvua ilikuwa inanyesha na wanakijiji walichimba mitaro kuelekeza maji kisimani wakidhania chuo huo angeogelea iwapo kisima kingejaa.
"Tuliwaambia angekuwa amekufa maji kufikia wakati huo," afisa mkuu mlinzi wa msitu Suresh Wadekar amesema.
Badala yake, Wadekar anasema aliamua kwamba chui huyo alihitaji kupumzika kwani alikuwa anapumua kwa nguvu.
Haki miliki ya pichaWIKIMEDIAImage captionNdege ya Kuwait iliyokataa kumbeba raia wa Israel
Mahakama nchini Ujerumani imeamua kuwa shirika la ndege la Kuwait lilikuwa na haki ya kukataa kumbeba raia wa Israel.
Uamuzi huo imegawadhabisha makundi ya wayahudi wanaosema kuwa unahalalisha ubaguzi dhidi ya wayahudi.
Shirika la ndege la Kuwait lilifuta tiketi ya abiria hiyo kutoka Frankfurt kwenda Bangkok.
Mahakama ya Frankfurt ilisema kuwa shirika hilo lilikuwa linafuata sheria za Kuwait amabzo hazitambui taifa la Israel.
Ilisema haikuwa na uwezo wa kuamua kuhusu sheria ya Kuwait na kuwa sheria za Ujerumani zinaamua katika masuala kuhusu ukabila, dini lakini sio kwa uraia.
Nathan Getlbart, wakili wa abiria huyo aliutaja uamuzi huo wa mahakama kama pigo kwa demokrasia na kwa Ujerumani kwa ujumla.
Baraza la wayahudi nchini Ujerumani lilisema kuwa ni jambo lisilokubalika kuwa kampuni ya kigeni inayofanya kazi kwa misingi ya ubaguzi dhidi ya wayahudi, itaruhusiwa kufanya biashara nchini Ujerumani.
"Tunaiomba serikali kuhakikisha kuwa visa kama hivyo havitokei siku usoni," alisema meya ya Frankfurt Uwe Bekcer.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMnangagwa amekuwa miongoni mwa waliotarajiwa kumrithi Mugabe
Imekuwa siri ya wazi nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kuwa Emmerson Mnangagwa angechukua nafasi ya Robert Mugabe na kuwa rais.
Lakini Bwana Mugabe alionekana kucheza na hisia zake- wakati mwingine akimpandisha cheo ndani ya chama tawala cha Zanu- PF na serikalini na kuongeza tetesi ya yeye kuwa mrithi mtarajiwa lakini baadaye alishushwa cheo baada ya Mnangagwa kuonekana kuonesha nia zake mapema mno.
Baada ya kutenguliwa, imeonekana kama subira ya mwanaume huyo maarufu kama "mamba" hatimaye imeisha. Baada ya Rais Mugabe kumtengua na kumshutumu kwa mfisadi, wafuasi wake na vikosi vya usalama waliingilia kati kwa niaba yake.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMkuu wa majeshi ya Zimbabwe Constantino Chiwenga (kushoto) ni rafiki wa karibu wa Mnangagwa
Mnangagwa alisaidia kuongoza vita vya kupigania uhuru vya Zimbabwe na baadaye kuwa jasusi mkuu wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.
Amekanusha kuhusika wowote katika mauaji hayo na kuilaumu jeshi.
Hata hivyo, hamna matumaini kuwa vitendo vya kukiuka wa haki za binadamu vitasitishwa chini ya utawala wake. Wakosoaji wake wanasema Mnangagwa ana damu mikononi mwake.
Anajulikana kama "mamba" sababu ya kizimu cha jamii yake; jina ambalo linaokenana kumfaa.Kwa maana hiyo, wafuasi wake hufahamika kama "Lacoste"
Emmerson Mnangagwa ni nani?
•Anajulikana kama "mamba" sababu ya kizimu cha jamii yake. , wafuasi wake wanafahamika kama "Lacoste"
•Alipata mafunzo ya jeshi nchini China na Misri
•Aliteswa na vikosi vya Rhodesia baada ya mashambilizi yake ya kiaina
•Alisaidia kuongoza kupigania uhuru nchi ya Zimbabwe miaka ya 70
•Alikuwa mjasisi wa nchi wakati wa mgogoro wa ndani kwa ndani ambapo maelfu wa wananchi waliuwawa.
•Anaojulikana lama muunganishi baina ya jeshi, idara ya ujasisi na chama cha Zanu- PF
•Anatuhumiwa kwa kuwa nyuma ya mashambilio dhidi ya wafuasi wa upinzania baada ya uchaguzi wa 2008
Haki miliki ya pichaAFPImage captionWalipigania uhuru Zimbabwe miaka ya 1970 wametawala siasa za nchi hiyo
Wale waliopigana katika vita ya miaka 70, kama Bw. Mnangagwa, wamehodhi madaraka kwa muda mrefu nchini Zimbabwe,huku wakiogopa kupoteza vyeo vyao kama Grace Mugabe angemritihi mume wake,kwa hio waliingilia kati.
Wakati rafiki wake wa karibu , Jenerali Constantino Chiwenga alionya dhidi ya 'vitendo vya vinavyolenga kuwatoa wanachama waliopiginia uhuru wa taifa' ilikuwa wazi kwamba alikuwa akizungumzia kufukuzwa kazi kwa Mngangagwa.
Uhusiano na Congo
Bw Mnangagwa alizaliwa mkoa wa kati wa Zvishavane na anatokea jamii ya Karanga iliyo jamii kubwa zaidi katika kabila ya Washona.
Wakaranga ni wa kundi kubwa la Washona na wengi wanahisi ni zamu yao kuingia madarakani kufuatia miaka 37 ya kutawaliwa na kundi la Zezuru atokaye Mugabe.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionWanajeshi wa Zimbabwea waliingilia kati mzozo DR Congo kuisaidia serikali
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa mataifa wa mwaka 2001, Bw Mnangagwa alionekana kama 'mhandisi wa shughuli za kuingiza fedha za Zanu-PF.'
Hii kwa kiasi kikubwa inahusisha operesheni za jeshi la Zimbabwe na wafanyabiashara katika Jamuhuri Ya Kidemokrasia ya Congo.
Majeshi ya Zimbabwe yaliingilia mzozo wa Congo kwa upande wa serikali, kama ilivyo nchi nyingine, wametuhumiwa kuutumia mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo kuiba utajiri wa maliasili wa nchi hiyo kama vile Almasi, dhahabu a madini mengine.
Lakini licha ya mchango wa kukipatia chama fedha, Bwana Mnangagwa, ambaye ni mwanasheria aliyekulia Zambia, sio mtu anayependwa sana na watu wenye vyeo na wasio na vyeo katika chama chake.
Mmoja wa Maveterani wa vita nchini Zimbabwe, ambaye alifanya naye kazi kwa muda mrefu, anaweka wazi kwa kumuelezea kuwa ni mtu katili.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMnangagwa alijipatia sifa zake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka ya 1980 kati ya chama cha Zanu chake Robert Mugabe (kushoto) na Zapu chaJoshua Nkomo (kulia)
Afisa mwingine wa ZANU PF aliuliza swali lenye mvuto, wakati alipotaka kujua kuhusu mtazamo wa Bwana Mnangagwa '' Unadhani kuwa Mugabe ni mbaya. Lakini ulifikiri kuwa yoyote atakayekuja badala yake anaweza kuwa mbaya zaidi?''
Mgombea wa upinzani ambaye ambaye alimshinda Bwana Mnangagwa katika kampeni za ubunge mwaka 2000, katika eneo la Kwekwe, Blessing Chebundo anaweza pia kukubaliana kwamba mpinzani wake siye mtu wa amani.
Wakati wa Kampeni kali, Bwana Chebundo alinusurika kifo baada ya vijana wa chama cha ZANU-PF, ambao walimteka na kummwagia petroli, lakini hata hivyo hawakufanikiwa kumchoma.
Ukatili
Sifa za kutisha za Bwana Mnangagwa zilianza wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka miaka ya 80 kati ya chama cha Rais Mugabe cha Zanu na kile cha Joshua Nkomo cha Zapu.
Kama Waziri wa Usalama wa Taifa wa Zimbabwe, Bwana Mnangagwa alikuwa akihusika na Idara ya Usalama wa Taifa, ambayo ilikuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na jeshi kukikandamiza chama cha Zapu.
Maelfu ya raia wasio na hatia, wengi wakiwa kabila la Ndebele, ambao ndio walioonekana kama wafuasi wa Zapu, waliuawa kabla ya vyama hivyo viwili kuungana na kuunda Zanu-PF.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMnangagwa hapendwi sana na watu wanaofuata sera za Zanu-PF
Miongoni mwa mambo ya ukatili yaliyofanyika ni pamoja na wanavijiji kulazimishwa kucheza huku wakiwa wamenyooshewa bunduki, wakati wa mazishi ya jamaa zao na maneno ya kumuunga mkono Mugabe.
Licha ya makubaliano ya umoja yaliyofikiwa mwaka 1987, bado majeraha ya maumivu yangali yapo. Na watu wa Kabila la Matebele pengine wanaweza kukaidi kumuunga mkono Mnangagwa katika kinyang'anyiro cha Urais.
Amepata Mafunzo China
Bw Mnangagwa ana wafuasi wengi ya waliokuwa katika wakiongoza kampeni ya vita dhidi ya wakulima weupe na wapinzani kutoka mwaka 2000.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionZimbabwe ilipigana vita vya msituni kabla ya kujipatia uhuru 1980Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionGrace Mugabe (kulia) anaonekana kukumbana na kisiki akikabiliana na Bw Mnangagwa
Wanamkukmbuka kama mmoja wapo wa wanaume,ambaye baada ya mafunzo ya kijeshi China na Misri,alioongoza vita vya kupigania uhuru vya 197.
Maelezo rasmi ya Bw Mnangagwa ni kwamba alikuwa mhanga wa ukatili uliotekelezwa na serikali iliyoongozwa na Wazungu katika taifa la zamani la Rhodesia mwaka 1965.Hii ni baada ya yeye na 'kundi la mamba' alilokuwa analiongoza walisaidia kulilipua treni iliokuwa karibu na eneo la Fort Victoria(ambayo sasa ni Masvingo).0.