Friday, November 17

Mbunge Heche asema polisi wanakusudia kumkamata



Dodoma. Polisi wanaoelezwa kutoka mkoani Morogoro wako eneo la Bunge ikielezwa kuwa wanakusudia kumkamata Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Heche, zimesema polisi hao wanamhitaji ili apelekwe Morogoro.
Heche leo Ijumaa Novemba 17,2017 amesema anaamini Spika Job Ndugai hataruhusu jambo hilo.
"Nimepewa wito kuwa natakiwa nikahojiwe Morogoro. Nimepokea wito huu na tayari nao wako hapa. Siamini kama Spika ataruhusu hili," amesema Heche.
Mbunge huyo amesema hajui kosa alilotenda, isipokuwa anatakiwa kuhojiwa kwa kauli alizotoa Machi mwaka huu alipomsindikiza Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali alipotoka gerezani.

No comments:

Post a Comment