Friday, November 17

Raila atua Nairobi, polisi wakifukuza wafuasi wake


Nairobi, Kenya. Pamoja na ulinzi mkali uliowekwa kuzuia wafuasi wa Nasa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyetta (JKIA) baadhi wamemudu kufika ili kumpokea kiongozi wao Raila Odinga akitokea katika ziara ya siku 10 nje ya nchi.
Raila aliyekwenda Marekani kulalamikia jinsi ulivyofanyika uchaguzi mkuu wa marudio kwa kura ya urais nchini Kenya alitua JKIA saa 5:00 asubuhi.
Ndege iliyokuwa imembeba Raila ilitua wakati polisi wakipambana na wafuasi wake ambao walikuwa wakihaha kuingia ndani ya kiwanja hicho kilichokuwa chini ya ulinzi mkali hali iliyosababisha kupambana na polisi.
Licha ya ulinzi huo na moshi wa mabomu ya machozi wafuasi wa Nasa wapatao 200 wakiwemo wanawake walifanikiwa kupita utepe uliowekwa na vyombo vya usalama na wakaingia hadi ndani ya uwanja.
Helikopta ya polisi ilikuwa ikizunguka juu ya uwanja huo huku magari ya maji ya kuwasha na magari ya maalumu ya kusafisha njia yalikuwepo uwanjani hapo na yalitumika kuzima moto wa matairi.
Jana Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na mwenzake wa Rauaraka TJ Kajwang na mwanasiasa wa Starehe Steve Mbogo walikamatwa na polisi.

No comments:

Post a Comment