Mnamo Julai 19, 2012, Anand Bora alipokea simu isiyo ya kawaida saa mbili asubuhi na kufahamishwa kwamba chuo alikuwa amekwama kwenye kisima katika kijiji kimoja jimbo la Maharashtra, magharibi mwa India.
Bw Bora alikimbia kwenye kijiji hicho cha Bubali na kupiga picha operesheni ya zaidi ya saa tatu unusu ya walinzi wa msitu na wanakijiji wakijaribu kumuokoa chui asife maji kisimani.
Ni mwalimu lakini mpiga picha na alipiga picha za kipekee siku hiyo.
Katika moja ya picha hizo, chui huyo kuwa anaonekana akitazama juu kuwaangalia wale waliokuwa wanamuokoa.
Picha hizo ilishinda tuzo ya upigaji picha wa wanyamapori nchini India wiki iliyopita.
Ushindi wake umeibua maswali kuhusu yaliyojiri wakati wa uokoaji huo.
Picha hiyo ya miaka mitano iliyopita ni ya kipekee kwani mara nyingi wanyamapori hushambuliwa na kuuawa na wakazi.
"Chui huyo alipotazama juu, anaonekana kuhisi kwamba hatungemuumiza, kwamba tulikuwa tunajaribu kumuokoa," Bw Bora ameambia BBC.
Maafisa wa msitu walipofika, wanakijiji waliwafahamisha kwamba chui huyo alikuwa ameogelea kisimani kwa saa 25 akijaribu kujizatiti asizame.
Mvua ilikuwa inanyesha na wanakijiji walichimba mitaro kuelekeza maji kisimani wakidhania chuo huo angeogelea iwapo kisima kingejaa.
"Tuliwaambia angekuwa amekufa maji kufikia wakati huo," afisa mkuu mlinzi wa msitu Suresh Wadekar amesema.
Badala yake, Wadekar anasema aliamua kwamba chui huyo alihitaji kupumzika kwani alikuwa anapumua kwa nguvu.
Akisaidiwa na wanakijiji, walirusha matairi mawili yaliyofungwa kwenye vipande vya mbao na chui huyo akapumzika juu yake,.
Kisha walirusha kitanda ambacho walikuwa wamekifunga kwa kamba na chui huyo aliruka na kuketi kitandani.
Walimuinua mnyama huyo hadi juu.
"CHui huyo alipofika juu, aliruka mbio na kutorokea msituni. Yote yalifanyika kwa muda mfupi sana," anasema Bw Bora.
No comments:
Post a Comment