Maafisa wa polisi wakilinda doria katika mbio za nusu -marathon mbele ya Kanisa la Berlin, Berlin, Ujerumani, April 8, 2018.
Vyombo vya usalama nchini Ujerumani vimewakamata watu sita Jumapili wakidaiwa kujihusisha na mpango wa kufanya shambulizi linalofungamana na siasa kali wakati wa michezo ya Berlin ya nusu-marathon.
Katika tamko la pamoja, waendesha mashtaka na polisi wamesema, “Kulikuwa na ishara zilizojificha kuwa wale waliokamatwa, umri kati ya miaka 18 na 21, walikuwa wanashiriki katika maandalizi ya kutenda jinai hiyo wakati wa michezo hiyo.”
Gazeti la German daily Die Welt mara ya kwanza liliripoti kuwa polisi walikuwa wamefanikiwa kuzuia mpango wa shambulizi lililokuwa likiwalenga watizamaji wa mbio hizo na washiriki wa michezo hiyo kwa kutumia visu.
Gazeti hilo pia limeripoti washukiwa wakuu hao kwa namna fulani walikuwa wanafahamiana na Anis Amri, mkimbizi mwenye asili ya Tunisia ambaye aliuwa watu 12 alipoteka lori moja na kuparamia kundi kubwa la watu waliokuwa katika soko la Krismas huko Berlin Disemba 2016.
Kukamatwa kwa watu hao kumekuja baada ya jeshi maalum la polisi la Ujerumani kuendesha msako katika nyumba za washukiwa wa kikundi cha mrengo wa kulia cha Berlin, wakipekua iwapo kuna silaha, Ofisi ya serikali kuu ya mwendesha mashtaka Ujerumani imesema.
Vyombo vya usalama hata hivyo havikueleza iwapo matukio hayo mawili yanamafungamano.
Kanisa la mchungaji Kakobe's mjini Dar es Salaam, Tanzania
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema yeye ni raia wa Tanzania na yule “anayesema mimi sio raia wa Tanzania aniambie ni raia wa nchi gani.”
Askofu Kakobe ametoa kauli hii Jumatatu baada ya kutoka kuhojiwa ofisi ya uhamiaji ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa takriban saa tatu.
Amesema inawezekana kuwa uhamiaji ina nia njema, lakini amehoji ni “kwa nini sasa, kwa nini wanahojiwa watu fulani wa kutoka eneo fulani la Kigoma. Mbona hatujasikia watu kutoka Dodoma, Kaskazini wakihojiwa.”
Vyanzo vya habari vimesema kuwa Askofu Kakobe ametakiwa kuacha hati yake ya kusafiria ili iweze kuwasaidia kupata taarifa zake muhimu huku yeye akisisitiza “hiki wanachokifanya kina tia shaka.”
Polisi nchini Ujerumani walizingira eneo la tukio la basi dogo lililowaparamia watu waliokuwa wanatembea kwa miguu.
Watu wasiopungua wanne wameuawa baada ya basi dogo kuligonga kundi la watu waliokuwa wakitembea kwa miguu katika mji wa Muenster, Ujerumani Jumamosi mchana.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Ujerumani dereva wa gari hilo ni Mjerumani mwenye matatizo ya kisaikolojia.
Polisi wakifanya ukaguzi katika eneo ambako gari limegonga watu na kusababisha vifo vya wanne na 20 kujerihiwa.
Kati ya wale waliokufa katika tukio hilo ni dereva mshukiwa, aliyejipiga risasi akiwa ndani ya gari hilo kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi.
Nalo gazeti la Sueddeutsche Zeitung limesema maafisa wanaamini hapakuwa na lengo la ugaidi katika tukio hilo.
Dereva huyo anaaminika kuwa ni Mjerumani mwenye umri wa kati aliyekuwa na matatizo ya kiakili.
Gazeti la Sueddeutsche pia limeripoti nyumba ya mshukiwa ilikuwa ikakaguliwa kutafuta uwezekano wa kuwepo na vilipuzi.
Hata hivyo maafisa wa serikali ya Ujerumani walikuwa bado hawajasema ni nini wanadhani lilikuwa lengo la tukio hilo.
Msemaji wa Polisi Andreas Bode amesema mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wamesema watu wengine waliondoka kwenye gari baada ya kugonga.
Shirika la habari la Ujeurmani DPA, liliripoti kwamba mashuhuda walizungumzia juu ya watu wawili waliokuwemo ndani ya basi hilo mbali na dereva na kwamba uchunguzi bado unaendelea.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema Jumatatu kuwa mazungumzo ya kibiashara kati yake na Marekani ni vigumu kufanyika katika hali hii ya mvutano unaoendelea.
Maoni hayo yaliyotolewa na msemaji wa wizara hiyo Geng Shuang wakati akiwapa muhtasari waandishi wa habari juu ya hali ya mazungumzo hayo ambao umetolewa siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutabiri kuwa kutakuwa na suluhisho katika mvutano uliopo baina ya Marekani na China.
Shuang alikuwa anawaeleza waandishi juu ya ushuru uliowekwa kwa bidhaa zenye thamani ya mabilioni ya Dola za Kimarekani ambapo mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa kuliko yote duniani wanatishiana kuanzisha ushuru huo kutoka kila upande.
“China itaondosha vikwazo vya kibiashara kwa sababu ni jambo lililo sahihi kulitekeleza,” amesema Trump, bila ya kutoa maelezo ya moja kwa moja juu ya suala hilo.
Amesema: “Ushuru huo utakuwa wamaridhiano kati ya pande mbili na tutafikia makubaliano katika suala la haki miliki. Kuna mustakbali mwema kwa nchi zote mbili!”
Vyovyote itavyokuwa, Trump amesema kuwa yeye na Rais wa China Xi Jinping “wataendelea kuwa marafiki, bila ya kujali nini kimetokea katika mvutano wao wa kibiashara.
Tishio ambalo Washington na Beijing wametupiana katika siku za hivi karibuni limetikisa soko la hisa la biashara, na kuyumbisha mamia ya numbari za mwelekeo wa hisa hizo.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionRais wa zamani wa Afrika Kusini,Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika Kusini anayeshtakiwa kwa makosa ya rushwa inayohusishwa na mpango wa silaha wa mwaka 1990.
Mara baada ya Bwana Zuma kuwasili katika mahakama kuu huko Durban hapo jana kwa kipindi cha dakika 15,kesi yake ilihairishwa mpaka tarehe 8 mwezi Juni.
Bwana Zuma ambaye anakabiliana na mashtaka 16 ya ufisadi,rushwa ,udanganyifu aliofanya ili kujipatia fedha na utakatishaji wa fedha.
Bwana Zuma alilazimika kuachia madaraka yake mwezi februari licha ya kukataa kuhusika na kosa lolote.
Wafuasi wake walisambaa mjini wakiandamana kwa ajili yake huku wapinzani wake walilalamika kwamba mahakama inachukua muda mrefu kutoa hukumu.
Baada ya kesi hiyo kusikilizwa,Bwana Zuma aliwahutubia mkusanyiko wa watu waliomsindikiza mahakamani kutoka nyumbani kwake.
"Sijawahi kuona mtu anashtakiwa kwa uhalifu, alafu mashtaka yake yanafutwa lakini baada ya miaka kadhaa ,mashtaka hayohayo yanarejeshwa" ,Zuma alisema.
"Hizi ni njama za kisiasa"
Image captionWafuasi wa Zuma nje ya mahakama
Baada ya hapo Bwana Zuma aliongoza nyimbo na kucheza pamoja na wafuasi wake.
Image captionMamia ya askari pia yalikuwa yanalinda
Mpango wa silaha ulikuwa ni upi?
Mpango wa silaha ulifanyika mwaka 1999 mwaka ambao bwana Zuma alihama kutoka mkuu wa jimbo kuwa makamu wa rais.
Anashtakiwa kwa kukubali kuchukua malipo yasiyokuwa halali 783
Mshauri wake wa mambo ya fedha ,Schabir Shaikh alikutwa na hatia kwa kujaribu kuomba rushwa kwa niaba ya bwana Zuma kutoka katika kampuni ya silaha za Ufaransa na kosa hilo lilipelekea akafungwa jela mwaka 2005.
Kesi dhidi ya bwana Zuma ilifutwa muda mfupi kabla hajawania nafasi ya uraisi mwaka 2009.
Haki miliki ya pichaIKULU/TANZANIAImage captionRais John Pombe Magufuli akimpongeza aliyesimikwa kuliongoza jimbo kuu la kikatoliki la Arusha
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamehudhulia ibada rasmi kwa ajili ya aliyesimikwa kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amemuahidi Askofu Mkuu Isaac Amani, na viongozi wote wa madhehebu ya dini hapa nchini humo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na viongozi hao katika masuala mbalimbali.
Aki nukuu vifungu mbalimbali vya Biblia, rais huyo wa Tanzania amesisitiza umuhimu wa Watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini, Serikali na wanasiasa kudumisha amani, na kwamba Serikali anayoiongoza itakuwa tayari wakati wote kutoa ushirikiano katika kuhakikisha amani inakuwepo.
Haki miliki ya pichaIKULU/TANZANIAImage captionMke wa rais Magufuli , Mama Janeth Magufuli(kushoto) pia alipata fursa ya kumpongeza Mhashamu Isaack Amani
Katika risala iliyosomwa na Padre Alois Kitomari kwa niaba ya familia ya Mungu Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, imempongeza rais Magufuli kwa juhudi zake za kusimamia vizuri nidhamu ya utumishi wa umma na utendaji wa taasisi za umma, kukabiliana na ufisadi, uzembe na ubadhilifu wa mali za umma, vita dhidi ya rushwa, ujenzi wa viwanda, bandari na madini na uboreshaji wa sekta ya usafiri kwa kujenga reli ya kisasa, ununuzi wa ndege na ujenzi wa barabara.
Haki miliki ya pichaIKULU/TANZANIAImage captionRais John Magufuli pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasalimia mapadre wa kikatoliki waliohudhuria ibada ya kusimikwa kwa Mhashamu Isaack Amani kama askofu wa jimbo kuu la kikatoliki la Afrusha
Hatua ya rais Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kuhudhuria ibada hii ya kanisa katoliki nchini humo inaonekana kama ishara bora ya kurejesha uhusiano mwema na baadhi ya makanisa makuu ya kikristo likiwemo kanisa katoliki ambao wamekua wakiikosoa vikali serikali yake...Maaskofu waonya kuhusu Umoja na amani ya Tanzania
Haki miliki ya pichaIKULU/TANZANIAImage captionRaisJohn Pombe Magufuli akiwapungia mkono waumini na viongozi wa kidini wakati wa ibada ya kusimikwa kwa Mhashamu Isaack Amani kama askofu wa jimbo kuu la kikatoliki la Arusha Jumapili
Licha ya kukosolewa, rais Magufuli alipuuzilia mbali mbali waraka wa maaskofu uliotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka akisema hauna msingi wowote ule.Aliendelea kwa kusema pia kwamba mbona hakuna aliyetoa waraka wakati mauwaji ya Kibiti yakiendelea.
Rais Magufuli alisema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada za kiraia uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Majibu yake kwa waraka wa maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake, mawaziri, viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine, ambao amewasifu kwa kuendelea kutimiza majukumu yao...
"Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ndio maana tuko salama leo, ilifikia mahali hata kwenda Kibiti tu ni kazi. Hatukuona mtu yeyote analaani," alisema Dkt Magufuli...Magufuli akejeli waraka wa maaskofu Tanzania
Mhashamu Askofu Isaac Amani aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francis tarehe 27 Desemba, 2017 kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha na amesimikwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMlinzi wa amani nchini Mali, akilinda usalama
Kikundi cha kutetea haki za binaadamu nchini Mali kimeshusha mzigo wa lawama kwa jeshi la nchi hiyo kutokana na kitendo cha kutekeleza adhabu ya kifo kwa wafungwa kumi na wanne katikati mwa jiji la Dioura.
Jeshi la nchi hiyo liliarifu kuwa wafungwa hao walikamatwa Almamisi wiki iliyopita na kuuawa muda mfupi tu baadaye.
Ndugu wa marehemu, ambao wanatoka katika kundi la kabila la Fulani, wametoa maelezo kuwa, ndugu zao hawakuwa na nasaba yoyote na makundi ya vijana wenye msimamo mkali.
Jamii hiyo ya kabila la Fulani imelalamika kuwa hii si mara ya kwanza kuhusishwa na makundi yenye msimamo mkali wa kidini.
Wiki hii, harakati za kundi la haki za binaadamu la Amnesty International limearifu kuwa wanaume sita walikutwa wamekufa katika kaburi la halaiki mapema mwezi uliopita ambao walitiwa mikono na jeshi siku tatu nyuma.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionHarry Kane anaamini bao la ushindi la Spurs Jumamosi ugenini Stoke linafaa kuhesabiwa kuwa lake
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane amesema anaamini atamshinda nyota wa Liverpool Mohamed Salah na kutwaa tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia msimu huu.
Mshambuliaji huyo wa England amefunga mabao 24 msimu huu.
Hata hivyo, ameachwa nyuma na Salah ambaye ni raia wa Misri kwa mabao matano.
Kane, 24, anapigania kuwa mchezaji wa kwanza tangu Thierry Henry kuongoza kwa ufungaji wa mabao Ligi Kuu ya England kwa misimu mitatu mtawalia.
"Naamini ninaweza kufanya hivyo. Bado kuna mechi zilizosalia kuchezwa," Kane amesema.
"Bila shaka kama mshambuliaji, itakuwa vyema sana kuishinda buti ya dhahabu tena na nitaendelea kutia bidhii kuanzia sasa hdi mwisho wa msimu."
Kane ambaye amekuwa akiuguza jeraha la kifundo cha mfuu amerejea kucheza baada ya kupona.
Mshindani wake Salaha, 25, hata hivyo hakucheza debi ya Merseyside Jumamosi kutokana na jeraha la mtoki alilopata akichea Liverpool mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano ambapo waliwalaza Manchester City mechi ya mkondo wa kwanza robofainali.
Kane ana nafuu kidogo ukizingatia kwamba Spurs wamesalia na mechi sita za kucheza Ligi Kuu lakini Liverpool wana mechi tano pekee.
Na huenda bado akafaidika zaidi katika kupunguza mwanya kati yake na Salah iwapo atahesabiwa bao la ushindi dhidi ya Stoke Jumamosi, ingawa kituo cha wasimamizi wa mechi cha Ligi ya Premia siku hiyo kiliamua kwamba Christian Eriksen ndiye aliyefunga bao hilo.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionVikosi vya Umoja wa Mataifa vikilinda amani DRC
Kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.
Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimearifu kuwa Padri Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini na ndipo wakati mtu mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.
Tukio hilo lilijiri wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.
Taarifa zinadai kuwa muuaji huyo ni kutoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji