Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane amesema anaamini atamshinda nyota wa Liverpool Mohamed Salah na kutwaa tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia msimu huu.
Mshambuliaji huyo wa England amefunga mabao 24 msimu huu.
Hata hivyo, ameachwa nyuma na Salah ambaye ni raia wa Misri kwa mabao matano.
Kane, 24, anapigania kuwa mchezaji wa kwanza tangu Thierry Henry kuongoza kwa ufungaji wa mabao Ligi Kuu ya England kwa misimu mitatu mtawalia.
"Naamini ninaweza kufanya hivyo. Bado kuna mechi zilizosalia kuchezwa," Kane amesema.
"Lazima niendelee kuangazia uchezaji wangu. Siwezi kudhibiti anachofanya yeye.
"Bila shaka kama mshambuliaji, itakuwa vyema sana kuishinda buti ya dhahabu tena na nitaendelea kutia bidhii kuanzia sasa hdi mwisho wa msimu."
Kane ambaye amekuwa akiuguza jeraha la kifundo cha mfuu amerejea kucheza baada ya kupona.
Mshindani wake Salaha, 25, hata hivyo hakucheza debi ya Merseyside Jumamosi kutokana na jeraha la mtoki alilopata akichea Liverpool mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano ambapo waliwalaza Manchester City mechi ya mkondo wa kwanza robofainali.
Kane ana nafuu kidogo ukizingatia kwamba Spurs wamesalia na mechi sita za kucheza Ligi Kuu lakini Liverpool wana mechi tano pekee.
Na huenda bado akafaidika zaidi katika kupunguza mwanya kati yake na Salah iwapo atahesabiwa bao la ushindi dhidi ya Stoke Jumamosi, ingawa kituo cha wasimamizi wa mechi cha Ligi ya Premia siku hiyo kiliamua kwamba Christian Eriksen ndiye aliyefunga bao hilo.
Spurs walilaza Stoke 2-1. Mabao yote mawili yalihesabiwa kuwa ya Eriksen.
Kane anasisitiza kwamba mpira frikiki iliyopigwa na Eriksen ulimgusa begani kabla ya kumbwaga kipa wa Stoke Jack Butland na kuingia wavuni.
Spurs wamepanga kukata rufaa uamuzi huo wa kumpa kiungo huo wa kati kutoka Denmark bao hilo na badala yake wanataka lihesabiwe kuwa la Kane.
"Naapa kwa uhai wa binti wangu kwamba niliuguza mpira huo, lakini hakuna jambo jingine ninaloweza kulifanya," Kane amesema.
"Wakiamua kubadilisha, watabadilisha. Wakiamua kuamini msimamo wangu, watakuwa wameusikia msimamo wangu.
"Mambo ni vile yalivyo - muhimu zaidi ni kwamba tulishinda mechi.
Wafungaji mabao bora EPL kufikia 9 Aprili, 2018
- Mohamed Salah, Liverpool 29
- Harry Kane, Tottenham 24
- Sergio Agüero, Man City 21
- Raheem Sterling, Man City 16
- Jamie Vardy, Leicester 16
- Romelu Lukaku, Man Utd 15
- Roberto Firmino, Liverpool 14
- Son Heung-min, Tottenham 12
- Álvaro Morata, Chelsea 11
- Eden Hazard, Chelsea 11
- Glenn Murray, Brighton 11
- Riyad Mahrez, Leicester 10
- Christian Eriksen, Tottenham 10
- Alexandre Lacazette, Arsenal 10
- Wayne Rooney, Everton 10
- Luka Milivojevic, Crystal Palace 10
- Leroy Sané, Man City 9
- Sadio Mané, Liverpool 9
- Alexis Sánchez, Man Utd, Arsenal 9
- Anthony Martial, Man Utd 9
- Marko Arnautovic, West Ham 9
- Gabriel Jesus, Man City 9
- David Silva, Man City 8
- Dele Alli, Tottenham 8
No comments:
Post a Comment