Tuesday, April 10

Rais Magufuli ahudhuria ibada ya askofu wa kikatoliki Mhashamu Isaack Amani

Rais Magufuli pamoja na Mhashamu Isaack AmaniHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionRais John Pombe Magufuli akimpongeza aliyesimikwa kuliongoza jimbo kuu la kikatoliki la Arusha
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamehudhulia ibada rasmi kwa ajili ya aliyesimikwa kuwa Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Mtoto Yesu Jimbo Kuu Katoliki.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amemuahidi Askofu Mkuu Isaac Amani, na viongozi wote wa madhehebu ya dini hapa nchini humo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na viongozi hao katika masuala mbalimbali.
Aki nukuu vifungu mbalimbali vya Biblia, rais huyo wa Tanzania amesisitiza umuhimu wa Watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini, Serikali na wanasiasa kudumisha amani, na kwamba Serikali anayoiongoza itakuwa tayari wakati wote kutoa ushirikiano katika kuhakikisha amani inakuwepo.
JanethHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionMke wa rais Magufuli , Mama Janeth Magufuli(kushoto) pia alipata fursa ya kumpongeza Mhashamu Isaack Amani
Katika risala iliyosomwa na Padre Alois Kitomari kwa niaba ya familia ya Mungu Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, imempongeza rais Magufuli kwa juhudi zake za kusimamia vizuri nidhamu ya utumishi wa umma na utendaji wa taasisi za umma, kukabiliana na ufisadi, uzembe na ubadhilifu wa mali za umma, vita dhidi ya rushwa, ujenzi wa viwanda, bandari na madini na uboreshaji wa sekta ya usafiri kwa kujenga reli ya kisasa, ununuzi wa ndege na ujenzi wa barabara.
Rais Magufuli akiwasalimiaHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionRais John Magufuli pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasalimia mapadre wa kikatoliki waliohudhuria ibada ya kusimikwa kwa Mhashamu Isaack Amani kama askofu wa jimbo kuu la kikatoliki la Afrusha
Hatua ya rais Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kuhudhuria ibada hii ya kanisa katoliki nchini humo inaonekana kama ishara bora ya kurejesha uhusiano mwema na baadhi ya makanisa makuu ya kikristo likiwemo kanisa katoliki ambao wamekua wakiikosoa vikali serikali yake...Maaskofu waonya kuhusu Umoja na amani ya Tanzania
Rais John Pombe Magufuli aliwasalimia waumini wa kikatoliki JumapiliHaki miliki ya pichaIKULU/TANZANIA
Image captionRaisJohn Pombe Magufuli akiwapungia mkono waumini na viongozi wa kidini wakati wa ibada ya kusimikwa kwa Mhashamu Isaack Amani kama askofu wa jimbo kuu la kikatoliki la Arusha Jumapili
Licha ya kukosolewa, rais Magufuli alipuuzilia mbali mbali waraka wa maaskofu uliotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka akisema hauna msingi wowote ule.Aliendelea kwa kusema pia kwamba mbona hakuna aliyetoa waraka wakati mauwaji ya Kibiti yakiendelea.
Rais Magufuli alisema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada za kiraia uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Majibu yake kwa waraka wa maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake, mawaziri, viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine, ambao amewasifu kwa kuendelea kutimiza majukumu yao...
"Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ndio maana tuko salama leo, ilifikia mahali hata kwenda Kibiti tu ni kazi. Hatukuona mtu yeyote analaani," alisema Dkt Magufuli...Magufuli akejeli waraka wa maaskofu Tanzania
Mhashamu Askofu Isaac Amani aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francis tarehe 27 Desemba, 2017 kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha na amesimikwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski.

No comments:

Post a Comment