Tuesday, April 10

Dereva wa basi Ujerumani auwa 4, ajeruhi 20 na kujiuwa

Polisi nchini Ujerumani walizingira eneo la tukio la basi dogo lililowaparamia watu waliokuwa wanatembea kwa miguu.
Watu wasiopungua wanne wameuawa baada ya basi dogo kuligonga kundi la watu waliokuwa wakitembea kwa miguu katika mji wa Muenster, Ujerumani Jumamosi mchana.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Ujerumani dereva wa gari hilo ni Mjerumani mwenye matatizo ya kisaikolojia.
Polisi wakifanya ukaguzi katika eneo ambako gari limegonga watu na kusababisha vifo vya wanne na 20 kujerihiwa.
Kati ya wale waliokufa katika tukio hilo ni dereva mshukiwa, aliyejipiga risasi akiwa ndani ya gari hilo kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la polisi.
Nalo gazeti la Sueddeutsche Zeitung limesema maafisa wanaamini hapakuwa na lengo la ugaidi katika tukio hilo.
Dereva huyo anaaminika kuwa ni Mjerumani mwenye umri wa kati aliyekuwa na matatizo ya kiakili.
Gazeti la Sueddeutsche pia limeripoti nyumba ya mshukiwa ilikuwa ikakaguliwa kutafuta uwezekano wa kuwepo na vilipuzi.
Hata hivyo maafisa wa serikali ya Ujerumani walikuwa bado hawajasema ni nini wanadhani lilikuwa lengo la tukio hilo.
Msemaji wa Polisi Andreas Bode amesema mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wamesema watu wengine waliondoka kwenye gari baada ya kugonga.
Shirika la habari la Ujeurmani DPA, liliripoti kwamba mashuhuda walizungumzia juu ya watu wawili waliokuwemo ndani ya basi hilo mbali na dereva na kwamba uchunguzi bado unaendelea.

No comments:

Post a Comment